Nataka kulipiza kisasi

Revenger

Member
Jan 28, 2020
12
9
Hakika una watu wanadharau humu duniani tena ya kiwango cha juu hivyo basi wanatakiwa watendewe sawa sawa na kiwango cha dharau yao.

Iko hivi, kuna kijana niliona ana mfatilia mke wangu nami nikamwonya zaidi ya mara tatu. Hivi karibuni nikathibitisha kuwa ni kweli ametembea na mke wangu.

Sasa kwa kuwa nilishamuonya na hakusikia wala kuelewa, nataka nimfanyie jambo liwe kumbukumbu maishani mwake.

Kwa huyu mwanamke yeye ameshapata anachostahili.

Nikiwatazama wanangu naumia sana maana wanaenda kuishi maisha wasiyostahili hata kidogo.

Kwa maelezo hayo nipo tayari kutumia chochote ili tu lengo langu lifanikiwe.

Tafadhali, nishauri nini nimfanyie huyu ndugu kwa uzito uleule alionitendea mimi.
 
Nikiwatazama wanangu naumia sana maana wanaenda kuishi maisha wasiyostahili hata kdg.

.

Umeshaweka mpango sawa namna ya watoto wako watakavyoishi na kusoma kwa kipindi chote ambacho hautakuwepo? ( kwenye kisasi unaweza ishia jela au kaburini).

Hakikisha unakamilisha taratibu zote juu ya hao watoto, umeacha hela kwenye account kwa ajili ya chakula, malazi na ada. Na hiyo nyumba tafuta msimamizi ambaye ni mwaminifu.

Kama hauna nyumba, hela za kutosha achana na mambo ya visasi utatesa watoto wako.
 
Hebu jiulize tena do they deserve your precious time! Muda ambao unapanga haya ni wa thamani sana,tulifundishwa hakuna kitu kinachokuumiza ila vile unakipokea! Tathmini tena mtazamo wako kwa hiyo hali.
Kuna wakati huwa wasalitiwa wanafikiri waliowasaliti wanaenjoy saaaanaaa, au wanakomoa mtu, au anafanya sababu ya madhaifu ya mwenzie, na hicho ndiyo kinachowaumiza,no usaliti has nothing to do with you, but all about them! Kumbuka huko nje wao pia hukutana na majuto, maumivu, rejections nk
At least ukikumbuka haya machache it will easy your pain.
Calm down brother it is not worth it!!
 
Mtu ambaye yupo tayari kuiharibu nyumba(familia) yako ni adui yako, tena ni adui mkubwa sana.

Hata mimi, atakayejaribu kuiharibu familia yangu ambayo natumia nguvu kubwa sana kuijenga, lazima aumie, hakika ataumia tu. People don't know that we go through sleepless nights just to make sure our families live well, wanataka kuteleza kwenye ganda la ndizi.

Do him good brother, teach him a good lesson that he will cherish for the rest of his life. Hata shetani alimuomba Mungu ili akamdhuru Ayubu, go for it brother.
 
Sijawahi kufikiria kufanya kitu kibaya kwa yoyote ksbb ya mke wangu kucheat. Wala usipanic. Jitahidi sana kujituliza,usiwe na haraka. Fanya tu mpango wa kuhakikisha,uwe na ushahidi. Fanya kuwafumania au mke wako akiri mbele za watu wengine kama ushahidi. Hatua ya pili muache kwa amani mkeo. Ikibidi mgawie hata baadhi ya vitu mlivyotafuta nae. Ninachokiamini mwanamke kampenda nae yule mwizi wako,haina haja uende jera ksbb ya mapenzi tu. Wewe msahau kabisa. Nakuhakikishia baada ya kumuacha kwa amani MUNGU ndie atahangaika nao,atakulipia kwa wakati usioujua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika Kuna watu wanadharau humu duniani tena ya kiwango cha juu hivyo basi wanatakiwa watendewe sawa sawa na kiwango cha dharau yao.

Iko hivi, Kuna kijana niliona ana mfatilia mke wangu nami nikamwonya zaidi ya mara tatu. Hivi karibuni nikathibitisha kuwa ni kweli ametembea na mke wangu.

Sasa kwa kuwa nilishamuonya na hakusikia wala kuelewa, nataka nimfanyie jambo Liwe kumbukumbu maishani mwake.

Kwa huyu mwanamke yeye ameshapata anachostahili.

Nikiwatazama wanangu naumia sana maana wanaenda kuishi maisha wasiyostahili hata kdg.

Kwa maelezo hayo nipo tayari kutumia chochote ili tu lengo langu lifanikiwe.

Tafadhali, nishauri nini nimfanyie huyu ndugu kwa uzito ule ule alionitendea mimi.
Tatizo halipo Kwa mke wako. Tatizo ni wewe mwenyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom