Nataka kukopa Shilingi milioni 5 nianze biashara

Sikushauri kufungua Duka hata kidogo,Duka la mahi taji ya nyumbani huwezi toboa ,kwanza ili upate faida kidogo linatakiwa kuuzwa na mtu mmoja tena mwaminifu

Wewe unatumia mkopo alafu unamwajiri mtu,na ukiwa unaingia Hesabu zikienda kombo jibu ni jepesi tulikuwa tunauza wote ,ndio njia Rahisi ya kukuibia

Kumbuka hata kama ni la familia anatakiwa muuzaji mmoja kwani tumetofautia mahitaji MF: ukiuza wewe jioni unaweza sema ngoja nichukua 5000 nijipongeze kwa chochote kumbe asubuhi kijana naye alitumia 10000 kuhonga/kununu chchote kwa chinga/ alimtumia Mzazi au kajiwekea malengo.wife pengine akaingia ata lisaa labda kijana alienda kununua mzigo akachukua naye 500 ya kusuka au kuongezea hitaji lake,Mtoto akisoma gepu ya kula Shule hata 1000, kumbe kwa siku mshatumi Hela nyingi bado Yale ya lazima ,Usafi ,kodi ,halmashauri usafi,umeme ,vocha n.k

Tafuta biashara ata mbaya mtaji mdogo kipato kikubwa ata kuuza Mkaa au unanunua mashine ya Kutengeneza Mkaa kwa kutumia matakataka kazi ambayo hesabu zinajulikana ua mgahawa n.k

Kuna jamaa ana chaneli yake ya Mgahawa mahali akiwaachia vijana kila siku anapitia Elfu Themanini(80000) haina mjadala na hapo weo wameshajilipa.
Jiongeze mkuu Duka hutoboi kwanza yamekuwa mengi siku hizi kila Mtu kazi ni hiyo
Umenifikirisha sana mkuu, ngoja niwaze na kuwazua tena vzur nione nafanyaje.

Shukran kwa ushaur mzur
 
Kaka mawazo yangu ni kuwa
Biashara yoyote inatokana na experience hata kwenye kazi za kuajiri nikitu kinacho angaliwa

Biashara pia ina changamoto nyingi, sio lazima uweke 5M yote katika business moja na ndo maana tunasema au kushauri watu wafanye diversification of capital( yaani usiweke mayai yote katika kapu moja tawanya mayai au mtaji wako)
Mfano biashara ikienda mlama inamaana capital yako ya 5M iko mahala pabaya.


Usifanye biashara kisa Juma anafanya na anapata faida
Haujui nyuma ya pazia anachokifanya, biashara zinamambo mengi ukiacha kitu kama Location kinacho pelekea biashara kufanikiwa, kuna Customer care, know how ya business , experience ya biashara unayotaka fungua unayo, Muda wa usimamizi unao?, Gharama za uendeshaji unazijua yaani Operating Cost usije ukawa umeangalia tu kwa macho ukajiridhisha inabidi ufanye reserch mpk ya gharama na wateja kujua kwa wastani wanakuwepo wangapi katika location yako, biashara nyingine watu wanaloga na kufanya makafala so nakuomba ufanye biashara unayoipenda toka moyoni usifanye kwakua unahitaji kufanya ili mkono uende kinywani au ili usogeze maisha.

Sijajua uko Mkoa gani ila kama unataka biashara inayotoka kwa haraka naweza sema ni biashara ya vitu vya electronic accessories kama Simu ( najua na kufahamu unaelewa watumiaji wa simu ni wengi), lakini pia kuna biashara nimeiona watu wanafanya ni ya Taa za Solar ambazo wanatumia watu wa magengeni mbadala wa vibatali na chemli yaani Taa izo zinachagiwa kwa Jua au Umeme jioni wanakuja kodi kwako kwakuwa hawawezi vuta umeme mpk pembezoni mwa barabara na kwa siku wanalipia elfu 1 tu ambapo wanatumia saa moja mpka saa 5 usiku wanarejesha so unaweza ona ukipata watu 20 umeingiza tsh 20,000 per day na nibiashara ya muda mrefu zaidi ila pia biashara nyingine niya Chakula ( watu wanafanya kazi ili wapate kula na kulala mahala pazuri, biashara ya Money transaction


Ila biashara zote izo zinafanywa na watu so ili uweze kutake over ni lazima uende extra na kuadd value katika biashara yako ndipo utakapo weza toboa usipende copy and paste biashara be Unique

Nihayotu ndugu yangu
Amina kaka
 
Biashara ya duka kidgo nimeona inavofanya kazi japo kwel wafanyakaz wanafaidi kuliko mabos wao
 
Aliyesema hivi ndio ana roho mbaya 'Biashara Ya Mahitaji Ya Majumbani Ni Za Kizamani Na Hazina Mwendeldzo Na Hazifai Kabisa Kwa Kijana Anaefikiria Kwa Karne Ya 21'................
By the way sio watanzania wote ni masikini wa kutupa.
Sawa Mangi
 
Diot kabisa kwani wewe hauwezi enda bank ukakopa yani umemgeuza mwenzio fursa akope yeye aweke kwenye biashara yako, acha umak* na kupenda kitonga kama unaona bzness yako inatoka andika proposal au tengeneza business plan uwezi kosa Capital sio kuja subiri wenzako wakope pesa zao wewe uje ujisogeze
Una Akili Ndogo Sana. Nakupuuza
 
Ni miaka 2 na nusu ijayo, sio 5
Kama Kweli Una Nia Ya Mafanikio Wekeza Kwenye Biashara Yangu ( Parnership ) Kwa Kuwa Utakuwa Kwenye Makaratasi Yote Kisheria Na Utajua Kila Kinachoendelea Kwenye Kampuni.

Biashara Ya Mahitaji Ya Majumbani Ni Za Kizamani Na Hazina Mwendeldzo Na Hazifai Kabisa Kwa Kijana Anaefikiria Kwa Karne Ya 21.

Ukiwekeza 10 Milioni Kuna Uwezekano Kabisa Wa Kuzalisha Mpaka Milioni 1 Kwa Mwezi Wakati Kwa Duka La Kawaida Huwezi Kupata.

Kumbuka Ukikopa 10M NMB Utakuwa Ukikatwa 253,000 Kila Mwezi Kwa Miaka 5 Na Kwa Kuwa Mshahara Wako Ni Tsh 353,000 Utcakiwa Na Nini Kwa Kuishi Miaka 5 Ijayo ?

Kama Kweli Una Nia Ya Kutoka Kimaisha, Wekeza Kwangu Na Kampuni Itakuwa Inalipa Mkopo Wako Wakati Wewe Ukiwa Aidha Na Kipato Kile Kile Pamoja Na Umiliki Wa Kampuni Au Zaidi.

Ila Duka La Mazaga Tena Kwa Kumweka Mtu, Utajuta Kwa Miaka 5 Ijayo.
 
Milioni 5 ikiwa invested
Baada ya miezi mitatu Faida inaingia si chini ya Milioni 1
Inapofikia miezi mitano ya biashara toka ianze tutakuwa tumelipa full installment ya mkopo mzima
miezi saba inayofuatia utakuwa umepata faida umekula 15mil in you hands

baada ya hiyo miezi 12 ya biashara tunavunja mkataba unaendelea na shuguli zako na mambo yako nasisi tunaendelea na mambo yetu
tunaingia mkataba kisheria
project ni uhakika zaidi ya 98% na hizo 2% ni vikwazo vichache vinaweza kujitokeza kuifanya ikadelay kidogo


Pia badala ya kununua bodaboda na kufungua duka
nakushauri fungua huduma zakipesa tu
weka hela yote hapo
tigo pesa, mpesa na airtelmoney
biashara hizi ukiwa sehemu nzuri laini zote kwa pamoja baada ya miezi mitatu ya mwanzo unakuwa na uwezo wa kukunja laki 7 hadi 1mil as profit kila mwezi

sikushauri duka na bodaboda sababu ni biashara zisizokuwa na misingi imara i mean zikigoma zimegoma mazima haziwezi kujishikilia na ni vigumu kusave mtaji
ila kwa biashara ya pesa ikigoma still pesa yako ipo pale pale
risk management ya mtaji wako iko safe zaidi katika iashara ya hizo huduma za kifedha kuliko bodaboda na duka
 
Aliyesema hivi ndio ana roho mbaya 'Biashara Ya Mahitaji Ya Majumbani Ni Za Kizamani Na Hazina Mwendeldzo Na Hazifai Kabisa Kwa Kijana Anaefikiria Kwa Karne Ya 21'................

By the way sio watanzania wote ni masikini wa kutupa.
Nakubaliana naye aliyesema hivyo, mwenye mawazo ya kimkakati kweli hafanyi biashara ya Duka la mahitaji ya nyumbani...Biashara niile inayo Scale na kukua binafsi hakuna biashara nitakuja ifanya kama hii ya duka.
 
waalimu mna matatizo gani nyie kila mtu anaweza kuwageuza chambo...elimu Elimu
Mimi Nashangaa Sana Mbongo Wewe Mwambie Utakuwa Tajiri Kesho, Jiunge Aim Global, Forever Living, Forex, GreenWorld Au Qnet Utayakamata Kibao.

Ila Wape Biashara Halali, Hapo Kila Mtu Atajifanya Ni Gwiji Wa Kukwepa Utapeli Na Mjanja Kama Sungura.

Tumerogwa Siyo Bure
 
Diot kabisa kwani wewe hauwezi enda bank ukakopa yani umemgeuza mwenzio fursa akope yeye aweke kwenye biashara yako, acha umak* na kupenda kitonga kama unaona bzness yako inatoka andika proposal au tengeneza business plan uwezi kosa Capital sio kuja subiri wenzako wakope pesa zao wewe uje ujisogeze
Kwani alipo mtapeli wapi mwenzio anatumia fursa aliyoiyona kwani sikuzote “Aliye na wazo zuri na muda hana pesa ila ambaye hana muda ndio anayopesa” sasa hawa watu wawili wakishirikiana wanafanya kitu wewe ambaye hujui kutumia fursa usiwakatishe tamaa wenzio wanaojua nini wanafanya...jamaa amesema akawekeze kwenye Biashara yake sasa shida ipo wapi hapo.
 
Kama Kweli Una Nia Ya Mafanikio Wekeza Kwenye Biashara Yangu ( Parnership ) Kwa Kuwa Utakuwa Kwenye Makaratasi Yote Kisheria Na Utajua Kila Kinachoendelea Kwenye Kampuni.

Biashara Ya Mahitaji Ya Majumbani Ni Za Kizamani Na Hazina Mwendeldzo Na Hazifai Kabisa Kwa Kijana Anaefikiria Kwa Karne Ya 21.

Ukiwekeza 10 Milioni Kuna Uwezekano Kabisa Wa Kuzalisha Mpaka Milioni 1 Kwa Mwezi Wakati Kwa Duka La Kawaida Huwezi Kupata.

Kumbuka Ukikopa 10M NMB Utakuwa Ukikatwa 253,000 Kila Mwezi Kwa Miaka 5 Na Kwa Kuwa Mshahara Wako Ni Tsh 353,000 Utcakiwa Na Nini Kwa Kuishi Miaka 5 Ijayo ?

Kama Kweli Una Nia Ya Kutoka Kimaisha, Wekeza Kwangu Na Kampuni Itakuwa Inalipa Mkopo Wako Wakati Wewe Ukiwa Aidha Na Kipato Kile Kile Pamoja Na Umiliki Wa Kampuni Au Zaidi.

Ila Duka La Mazaga Tena Kwa Kumweka Mtu, Utajuta Kwa Miaka 5 Ijayo.
Mjini shule watu wametajiwa hela mishipa imesimama
 
Dah mkuu kwa hiyo biashara yako ikipata hasara mnaanguka wote! Hujasema biashara yako ni ya nini na wala hujafunguka iko mkoa gani!
Hapo kuna issue ya kufanya due diligence ili ajue uwezo, uimara na sustainability ya biashara yako maana yawezekana biashara ikaonekana kwa juu juu kuwa ni nzuri lakini kukawa na madeni ambayo unatafuta mtu aweke pesa ukayalipe
Dunia Kote Ukiwa Na Hisa Kwenye Kampuni, Ikipata Hasara Na Wewe Unapata - Ikipata Faida Na Wewe Unapata. Ndivyo Ilivyo.

Mtu Anaekwambia Eti Ukiwekeza Utapata Faida Tupu Ni Tapeli, Labda Kwenye Fixed Deposits Za Bank !
 
Poor Mentality a.k. Low thinking capacity
Skuizi watu ni Kukopy biashara tu kuanzisha zao hawataki kabisa
Kuanzisha Biashara mpya kwani mahitaji ya binadamu wamebadilika kama sikuhizi binadamu wanalala juu ya miti kweli tunahitaji idea mpya ya kutengeneza miti nyumba, kama binadamu sikuhizi wanakula funza tutahitaji idea mpya ya kuzalisha funza...Kama mahitaji ni yaleyale kipya kinahitajikaje.

Huitaji idea mpya kutengeneza pesa EBay, Alibaba, Instagram, Alexpress, Kikuu, Jamiiforums, Clouds, Wasafitv, Infinix zote sio idea mpya ila zinatengeneza milioni ya pesa.

IDIOT
 
Mhh! Mbona hawa NMB wana makato makubwa hivi?
Mm ni mwalimu npo mbeya mjini na mshahara wang kwa sasa take hom ni kama 350 iv, nataka kukopoa NMB kiasi tajwa kwa ajili ya kufungua kibanda cha mahitaji ya kawaida ya majumbani, location nimepata nzur ila bado najiuliza kama ntatoboa.
NB: nategemea kuajiri mfanyakaz kwa sababu muda mwing wa mchana nakuwa Mazini na jion ndio ntakuwa na muda wa kuwa Kubandani

Naombeni kuwasilisha
View attachment 1226709
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom