Nataka kuja Tanzania kutafuta maisha naomba ushauri wenu

Huyo atakua kweli ni mzawa wa Tanzania ila kakulia Kenya, maana huko Kilifi ni pwani ya Kenya na ambapo wana undugu sana na Watanzania wa pwani na Zanzibar, wote huko huwa wamenyoosha Kiswahili sio kama sisi wa mikoani.
Namshauri huyu dogo kama ana uwezo wa kuzungumza Kingereza kama ilivyo kwa Wakenya wengi, basi fursa atapata kibao huko Bongo, nimeona Watanzania waliokulia Kenya baada ya kupata fursa ya kunyoosha kingereza, wakirudi Bongo hupata fursa nyingi sana maana kwenu huko kingereza full balaa, hivyo kumpata Mtz anaongea lugha zote mbili kwa ufasaha huwa adimu, na wale wachache hupata fursa za kila aina kuanzia kwenye utalii hadi kwenye ualimu.
Kawaida Tanzania hupambana kuzuia ajira kwa Wakenya kisa tunawafunika kwenye lugha ya malkia na ambayo mnaitegemea kwenye mambo mengi japo kwa shingo upande, ila sasa huwa haina namna ya kuwazuia Watanzania waliokulia au kusomea Kenya.
Hili tangazo hapa litakupa mwanga wa nini ninachokisema.....

View attachment 1500173
Haha hilo tangazo hakuna kitu kama hicho! La wanalao jambo.
 
Tanzania kuna mambo mengi ya kufanya ili maisha yasonge.

Tujulishe uwezo wako, kibiashara, ajira au kilimo.
 
Niko Dar es salaam
Dar ni fursa ya kila kitu.
Dar watu hawalali
Dar mzunguko wa hela ni mkubwa kuliko mikoa yote
Dar ina 10% ya population ya Tzania

Karibu Dsm
Vipi kuhusiana na biashara za kuagiza vitu kutokana nje..unauzoefu wowote hasa kwenye mambo ya tax
 
Kwasasa Hivi Jitahidi Urudi Tanzania Upate Kazi Nzuri
Nchi Imetulia, Tupo Salama Uchumi Wa Kati
Hongereni sana kwa kufika uchumi wa kati nasisi watu tukija huko kutakuwa na fursa nyingi
 
Habari za muda huu wanajamii forum wote.. poleni na mihangaiko ya maisha...naomba niende kwenye mada moja kwa moja:

Mimi ni mtanzania ambaye nimekulia kenya.. Niliondoka Tanzania kipindi nipo mdogo kabisa na kukulia Kenya maeneo ya kilifi kwani huku ndo nimepata elimu yangu yote huku hadi dakika hii naandika hapa nipo maeneo ya huku.

Sasa nimeona sio mbaya kwasasa kubadilisha mazingira ya kuishi hasa kwa ajili ya kutafuta opportunities sehemu nyingine mbali na nilipopazoea mawazo yangu yote kwasasa ni kurudi Tanzania nchi yangu nilipozaliwa kuja kuangalia opportunities na kuliendesha gurudumu la maisha.

Sasa ndugu zangu nilikuwa naomba ushauri kuhusu maisha ya huko hasa hasa opportunities za huko? usalama wa maisha huko? Urahisi na uhakika kwenye suala zima la transportation? hali ya hewa kwa ujumla ? pamoja na baadhi ya mambo na changamoto zake:
Karibuni sana ndugu zangu napokea ushauri wa aina yeyote.
Toka hapo Buguruni na uache kutuchora.
 
Karibu sana ndugu yetu ila ukija na ujuaji wa wakenya tunakurudisha huko bila barakoa wala sanitizer
 
Dar is the best of the best

Mwanza kibiashara iko vizuri, mji uliotulia unaishi kwa amani ukilinganisha na Dar vibaka, majambazi n.k, Mwanza watu wake ni wastaarabu tofauti na Dar, Mwanza ni kusafi ukilinganisha na Dar 🤭 Mwanza maisha easy ukilinganisha na Dar expensive, mwisho kabisa Dar mji wa kitapeli
 
Lakini wakati unaenda Kenya hukutuambia kwanini sasa ? ama umefanya uhalifu huko :cool::cool::cool:
 
Back
Top Bottom