Njoo hapa Bankok Thailand..fursa kibao, heshima rundo.kupata visa nenda Nairobi.kuna wa Nigeria na wa west kwa ujumla wengi sana hapa.maisha ni rahisi ambavyo huwezi kufikiria.usafiri, appartments, vyakula,biashara ni nyingi na hazina mikwara kama kwetu.wamachinga wamepewa nafasi kila kona..street hawkers na mama ntilie wa kutoka sehemu mbalimbali nje na thai wanashirikiana na wenyeji kufanya biashara.wenyeji wanaheshimu wageni ni balaa.ukishuka airport yao ya "subhanabhumi"utakaribishwa na bango kubwa"THE OPPORTUNITY HAVE LANDED WELCOME TO BANKOK"yaani wewe ni fursa umetua kwa hiyo unatakiwa kutumika.
Pia vijana wenzangu wenye kuwaza kufanya biashara za madini Bankok is the best place you can meet with international gemstones buyers
Njoo aise usiogope.mfano waweza pata appartment ye ye room 1 sebule, kitchen na toilet kwa 2500bhats.sawa na dola 80.bill za maji na umeme ni vichekesho.ni bhat 100 flat rate.gesi huku ndio kwao imeleta mapinduzi makubwa sana ya uchumi.watanzania tujiandaeni na ujio wa matumizi ya gesi yetu.tusiwaachie wahindi na wengine kutoka asia wa dominate sekta hii nikimaanisha biashara na fursa zinazotokana na gesi, biashara, gas stations zote ziwe za wazawa.katiba yetu itamke wazi mambo kama haya.ng'wabeja sana.