Nataka kufungua biashara Kariakoo, unanishaurije?

Stv Mkn

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
328
273
Wakuu,

Mimi nina mtaji wa shillingi million 4 nataka kufanya biashara na ndoto yangu ni kufanya biashara Kariakoo. Iwe biashara yoyote kati ya nguo, viatu, pochi, nguo za ndani au simu.

Katika utafiti wa awali nimeona kuna vijana pale wanakodisha ubavu (wenye mitaji mdogo kama mimi) na kuweka biashara zao maana fremu ni ghali sana, pia nilipata kule mtaa wanaouza simu nikaona kuna vijana wanakodisha shelfu ndogo za vioo badala ya duka zima kisha wanaweka simu .

Nilikuwa naomba mwenye uelewa na biashara ya kariakoo anipe ushauri, kuhusu ni bidhaa zipi zinatoka sana, uagizaji wake, namna ya kupata sehemu ya kuuzia kwa bei rahisi kwa sie wenye mitaji midogo bila kutapeliwa. Pia ushauri wowote ule ambao utanisadia.

Natanguliza shukrani kama ikiwezekana nipe mawasiliano nikutafute personally.
 
Nenda kwenye vikabati vya sim,kwa pesa hiyo kodi unalipa na biashara unafanya vizuri tu.
 
Poa mkuu nimekusoma. Sema nilitaka nipate ABC za hii biashara umu umu jf kama ingewezekana kabla sijaingia uko. Like mzigo unapata wapi kirahisi na unapataje, wateja wa kudumu wale wa kuwapelekea mzigo moja kwa moja na kipi kunatoka sana kati ya simu na vifaa vya simu vitu kama hivyo.
 
Wakuu,

Mimi nina mtaji wa shillingi million 4 nataka kufanya biashara na ndoto yangu ni kufanya biashara Kariakoo. Iwe biashara yoyote kati ya nguo, viatu, pochi, nguo za ndani au simu.

Katika utafiti wa awali nimeona kuna vijana pale wanakodisha ubavu (wenye mitaji mdogo kama mimi) na kuweka biashara zao maana fremu ni ghali sana, pia nilipata kule mtaa wanaouza simu nikaona kuna vijana wanakodisha shelfu ndogo za vioo badala ya duka zima kisha wanaweka simu .

Nilikuwa naomba mwenye uelewa na biashara ya kariakoo anipe ushauri, kuhusu ni bidhaa zipi zinatoka sana, uagizaji wake, namna ya kupata sehemu ya kuuzia kwa bei rahisi kwa sie wenye mitaji midogo bila kutapeliwa. Pia ushauri wowote ule ambao utanisadia.

Natanguliza shukrani kama ikiwezekana nipe mawasiliano nikutafute personally.
"Kila la kheri ndugu.. jaribu hiyo ya simu kwasababu nguo kila siku mitindo inabadilika badilika. unataka kufanya biashara ila siri ya biashara unaijua sawasawa? Biashara sio Mtaji tu..
 
Ndoto yako kufanya biashara kariakoo au kufanya biashara sehemu yoyote itakayoweza kukulipa?
 
Kwa muda huu Na Biashara ya simu popote pale sikushauri kufanya utapoteza Pesa yako, kipindi ni kigumu sana Kwa simu mpk mwezi wa 6 uishe, hapo Ingia.
 
Wakuu,

Mimi nina mtaji wa shillingi million 4 nataka kufanya biashara na ndoto yangu ni kufanya biashara Kariakoo. Iwe biashara yoyote kati ya nguo, viatu, pochi, nguo za ndani au simu.

Katika utafiti wa awali nimeona kuna vijana pale wanakodisha ubavu (wenye mitaji mdogo kama mimi) na kuweka biashara zao maana fremu ni ghali sana, pia nilipata kule mtaa wanaouza simu nikaona kuna vijana wanakodisha shelfu ndogo za vioo badala ya duka zima kisha wanaweka simu .

Nilikuwa naomba mwenye uelewa na biashara ya kariakoo anipe ushauri, kuhusu ni bidhaa zipi zinatoka sana, uagizaji wake, namna ya kupata sehemu ya kuuzia kwa bei rahisi kwa sie wenye mitaji midogo bila kutapeliwa. Pia ushauri wowote ule ambao utanisadia.

Natanguliza shukrani kama ikiwezekana nipe mawasiliano nikutafute personally.
Unajua mie naweza kusema kwamba kariakoo kwa sasa inawenyewe,New Comers ni tabu saana kutoka.

Na mfumo wa jiji unabadilika kila siku,hao unaosema wanaweka pembeni mwa duka la mhusika na kulipa kidogo,nao wana hali ngum
Kama unakumbuka kwamba mwaka jana,City walizuia kutundika nguo na bidhaa nje,hili lilikuwa pigo sana kwa machinga.Na kufanya maisha kutokuwa na uhakika.

4m ni nyingi sana kwa machinga.1m tu inatisha,ila kwa hali ya jiji inavyokwenda ni kwamba Machinga wengi watakuwa ni watu wasio na uhakika wa kesho wataamkaje.
Kwahiyo sikushauri saana kuingia huko,wale machinga ni vichwa ngum sana aisee,kila mtu mungu kampa uwezo wake.Yaani kama City wanakuja basi wao harufu wanaisikia,sasa wewe kama mgeni kila siku utakamatwa.

Pango kariakoo ni ghali,kuna mapango yanakaribia 2m,na rahisi ni 1m.
Ujue kwamba wale wenye vioski nao safari yao ipo njiani,na itatakiwa waliopo kwenye frames tu unless uwe nje ya Kariakoo au pembezoni ndio unaweza kuvuta pumzi kwa muda,ila maeneo ya kati kama pale Mtaa wa raha na mingine,aisee hutoki.
Na pia wale unaowaona wenye vibanda pale,ni kwamba wao wanasoko lao,sasa wewe unaweza pale ukawa unategemea mteja wa moja kwa moja itakuwa ngum saan,we angalia tu pale Kariakoo unaweza kukuta mtu anatoka mbioo anaenda duka fulani anachukua nguo kisha anarudi mbiooo anampa mteja.Yaani ni biashara fulani tata sana kwa mgeni.Na ndio maana nasema kariakoo kwa kijana kuanza pale ni kujidumaza sana.Dar kubwa kuna watu hadi tandika huko wanapiga pesa tu.

Ila sema tu kariakoo ni ujiko kwamba upo Center,lakini changamoto za pale ni ngum sana kwa mtaji mdogo,unless mtaji mkubwa wa frame nzima,na ukizingatia frames za chini siku hizi issue,watu wanapangishwa hadi kwenye ghorofa huko.Kuna kaka yangu anamaduka mawili ila moja limemshinda,sasa ndio ujue kwamba Kariakoo ni tofauti na unavyoiona.Watu wanaakili eneo lile kama mchwa.
Unawezakuona mtu anaduka na wateja hana lakini anakomaa,sasa mtu huyo utakuta anawateja kibaoo kutoka Zambian,Congo,Zimbambwe,nk,wnaomfanya aishi mjini.

Nakushauri tafuta maeneo ya Tandika kule kapige pesa,lile soko kubwa saana mkuu,Manzese,Soko La Mbagala na Mwenge.Maeneo yote hayo fursa kibao zipo
 
Mkuu nimekusoma vizuri sana.
 
Tuanze kwanza na eneo kigoli unacho zungumzia vingi kuanzia laki 3 hadi 5 kodi na kuna kitu kinaitwa kilemba inategemea na atakae kuuzia anataka shingap na si chini ya miez sita, meza za wamachinga ukipata mtu asie na tamaa elf tano kwa siku hapo inategemea na makubaliano unaweza lipia kwa miez 3 ama 6 ni vyote hivi bei inaongezeka ama kupungua kulingana na mtaa ulivyo changamka mfano Congo, Agrey, Mchikichi, raha square ni ghali, biashara za kufanya ni nyingi vitu vya kike vya bei rahisi ila vinahitaj uzoefu katika kuchagua mali inayo toka usije chagua mzigo usiotoka kila la kheri.
 
Back
Top Bottom