Waungwana Card zipo za aina Mbili
- Debit Card
- Credit card
Sasa hizo zinaweza kuwa either Visa, MasterCard, Discover, American-express etc, so kadi yeyote ambayo ni Debit/Credit napia kwa chini ikakuonesha kuwa ni Visa,MasterCard n.k ina weza kufanya online payment.
Issue ya kuibiwa online ipo sana lakini isikufanye uogope, kwa sababu huku sehem zingine bila online payments maisha hayaendi, so unatakiwa kufanya biashara na trusted sites kama Amazon, ebay, Airlines, Hotels,Brands zote kama nike, addidas n.k hyo ina tegemea na mahitaji yako. Atleast ukifanaya biashara na hizi campuni unakuwa na uhakika wa mkubwa sana kuwa taarifa zako zitakuwa safe.
Kuna option nyingine ya kutumia paypal, hapa unatoa taarifa zako za card kwa paypal tu, sehem zingine unanunua kwa kutumia account ya paypal ambayo ni email address yako na password tu , CRDB visa card inaweza kutumika kwa paypal vizuri kabisa. japo si wauzaji wote online wanatumia paypal, ebay wanatumia paypal vizuri kabisa na ninauhakika mahitaji yako mengi kama syo yote yatakuwepo ebay.com so jaribu paypal.com
Kila la Kheri