Rjohn usithubutu kuacha ualimu kuwa mbunifu utafanikiwa hakuna kazi utakayokuwa huru kama ualimu ni kazi gani ambayo ni ya kuajiriwa halafu unapata muda wa kufanya shughuli zako bila tabu unajipa likizo kiulaini jishughulishe usisubiri serikali ikutambue jitambue mwenyewe kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe
Siyo kweli!!!!
Hakuna kazi inayohitaji muda mwingi kama ualimu. Mwalimu anapaswa ajiandae kufundisha, atoe kazi na asahishe kazi ya kila mwanafunzi ili kupima/kutathmini kama kila mwanafunzi ameweza kufikia malengo ya somo. Mwalimu pia hufanya kazi zingine nje ya darasa hasa malezi katika nyanja mbalimbali mfano michezo, tabia/maadili nk. mwalimu husimamia usafi na shughuli nyingine kwa lengo la kumjenga mwanafunzi kiakili, kitabia/mwenendo na kiroho.
Watu wengi huishia kusema walimu wana muda mwingi wa kufanya mambo binafsi kwa sababu wanawaona walimu wanakaa bila kazi. Kimsingi walimu na watumishi wengi wa serikali hawatekelezi majukumu yao inavyotakiwa. Madhara ya walimu kutotekeleza majukumu yao kama inavyotakiwa tunayashuhudia... mfano wanafunzi kumaliza darasa la saba hawajui kusoma. kuandika na kuhesabu. Hali ya elimu sekondari pia inadidimia siku hadi siku.