Nataka kuachana na ualimu

Rjohn

JF-Expert Member
Feb 28, 2012
613
225
habari ndugu zangu wana jf! mimi ni mwanafunz wa mwaka wa 2 chuo cha Ualimu Mororogoro nasomea masomo ya HE(history na kiingereza) natarajia kuhtimu mwakan mwez wa tano! niliingia katka fan hii kutokana na mambo yangu mengne yote kugoma sa naomba kuulza na pengne kupata ushauri je kupitia chet changu cha diproma naweza kupata kaz nyngine tofaut na ualimu! au hata kama ntaendelea mbele kimasomo kupitia chet hcho nkabadili fan na nisiwe mwalimu tena! plz help me! kwa ushauri tu! thanx
 
ndupa

JF-Expert Member
Jan 25, 2008
4,405
0

je unajua maana ya ualimu?? kama hujui kwa nini ulienda?? je kwanin hutaki kwenda kufundisha wakati nchi ina upungufu wa waalim? je unataka wanafunzi wafundishwe na nani kama nyie wenye jukumu mnakumbia??
KWA USHAURI...
ukiwa na diploma unaweza kwenda degree ya kitu kingine hasa ya elimu na kama ukiwa na degree ya education atleast ina pay,na hata kama hutaki fundisha basi unaweza fanya ishu nyingine(japo itategemea ulisoma degree gani),na kama hiyo haitoshi unaweza pia chukua masters ya kitu kingine kabisa tofauti na education! naiman hayo ndo nliyonayo.....all the best!
 
Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Feb 12, 2012
10,645
2,000
unaweza kusoma BACHELOR YA BIZNESS STUDIES NA BA ZA ARTS usijali,,,ukibaki na ualimu hakyamungu utakufa MASKINI

Hapo nilipo-bold kiukweli tunahitaji kuwapa pongezi walimu wetu maana pamoja na yote lakini tupo hapa na wengine wanawashauri wenzao wakimbie fani
 
Visenti

JF-Expert Member
Jul 24, 2008
1,021
1,170
je kupitia chet changu cha diproma naweza kupata kaz nyngine tofaut na ualimu! au hata kama ntaendelea mbele kimasomo kupitia chet hcho nkabadili fan na nisiwe mwalimu tena! plz help me! kwa ushauri tu! thanx

Rjohn, tafadhali sana ukipata post ya ualimu nenda ukafundishe, ukiwa kazini utaweza kufanya maamuzi sahihi kuhusu mwelekeo upi uchukue.
 
Gilly

Member
Aug 6, 2009
87
95
By Rjohn

au hata kama ntaendelea mbele kimasomo kupitia chet hcho nkabadili fan na nisiwe mwalimu tena! plz help me! kwa ushauri tu! thanx

Mkuu asikutishe mtu! Walimu ndio kila kitu hata wakiwafisadi namna gani. Ndiyo kiboko ya nchi. Nakushauri maliza masomo yako, nenda ukafundishe na ukiwa huko utaondoka tu. Mifano iko mingi tu ukianzia na Nyerere mwenyewe, kisha jumlisha idadi kubwa ya wabunge, mawaziri kama Kawambwa, Kabaka, Mulugo, ma-RC kama Mahiza, kisha mimi nawafahamu wanasheria, maafisa utumishi, waragibishi wa maendeleo, maaskofu, mashekh, walio"join" benki, wajasiriamali, maafisa mipango wa Halmashauri na hata Serikali Kuu, mapolisi, na hata matapeli kibao ambao walianzia maisha na "kucheza na watoto darasani" tena darasa la shule ya msingi. Mimi mwenyewe nimestaafu "panono" tu huku nikiwa sijui kazi nyingine isipokuwa ya ualimu! Asikudanganye mtu.
 
mtzedi

JF-Expert Member
Dec 13, 2011
4,162
2,000
Kama una mtaji wa kutosha acha wala usisite,ila kama unajaribu kupima upepo itakula kwako ukisoma hizo kozi zingine ndo utapata ajira? Tanzania ya leo kupata ajira ni kazi kwelikweli unaweza ukakata tamaa ya kuishi. Chukua hatua:rofl:
 
mtamanyali

JF-Expert Member
Dec 6, 2011
1,158
2,000
ualimu ni janga, ila nakushauri nenda kafanye kazi ya kufundisha ili upate mtaji wa kujisomesha maana ukifika kule unaweza kupata mkopo wa kuweza kujisomesha ila usitegemee kufanya kazi hii,
 
kiwatengu

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
16,279
2,000
habari ndugu zangu wana jf! mimi ni mwanafunz wa mwaka wa 2 chuo cha Ualimu Mororogoro nasomea masomo ya HE(history na kiingereza) natarajia kuhtimu mwakan mwez wa tano! niliingia katka fan hii kutokana na mambo yangu mengne yote kugoma sa naomba kuulza na pengne kupata ushauri je kupitia chet changu cha diproma naweza kupata kaz nyngine tofaut na ualimu! au hata kama ntaendelea mbele kimasomo kupitia chet hcho nkabadili fan na nisiwe mwalimu tena! plz help me! kwa ushauri tu! thanx

ni afadhani uachane na hiyo fani kwasababu huiwezi na
hapo kwenye nyekundu ni ushahidi tosha..
 
Msingida

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
8,364
2,000
Kasome uchungaji au Ushehe maana unaonekana unataka kazi za kukutoa kimaisha.Huko ni sadaka kwa kwenda mbele.Sindio maisha unayoyataka?
Kama uliingia ualimu kwakuwa hukuwa na cha kufanya inaonyesha huna interest na fani hiyo.Unapoteza muda kwakuwa utahusisha anguko lako na ualimu wakati hata ungekuwa mhasibu wa benki bado yangekukuta.Tuliza akili,maisha ni wewe mwenyewe unavyo ya peleka
 
The secretary

JF-Expert Member
Jan 14, 2012
4,150
2,000
Rjohn usithubutu kuacha ualimu kuwa mbunifu utafanikiwa hakuna kazi utakayokuwa huru kama ualimu ni kazi gani ambayo ni ya kuajiriwa halafu unapata muda wa kufanya shughuli zako bila tabu unajipa likizo kiulaini jishughulishe usisubiri serikali ikutambue jitambue mwenyewe kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe
 
FreedomTZ

JF-Expert Member
Jul 18, 2012
1,104
1,250
Unachotafuta ni fedha/utajiri au kutumikia watanzania? Kama unatafuta utajiri ualimu haukufai
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom