Nataka kuacha hii kazi, Nisaidieni

Nataka kuacha hii kazi, Nisaidieni

kapumbiti kapumye

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2014
Posts
201
Reaction score
53
Ninafanya kazi Dar:

My gross salary: 610000;

Deduction is as follows:
NSSF (10%)= 61,000
PEYE = 65,700
HESLB (Education loan 8%) =48,800
CRDB loan=183,000
Worker union=12,200
BIMA YA AFYA = 10,800
Total deduction 381500
Net pay( take home) = 228500

228500 Ndio nauli, chakula, kodi ya nyumba na kila kitu dunia hii;
Nina miaka 31 lakini suala la kuoa halipo kabisa sababu ya kipato.
 
ukiwa bila kaz utalipaje deni? hebu funguka vizur.
 
Fungua kijibiashara hata kigenge cha nyanya mueke dogo ikiungizie sh2, kuliko kutegemea hyo ya mshahara tu,,
Na ukisubir kupata mshahara mkubwa ndo uoe utazeeka,,

Mi nakushauri tafuta mtu anaejua maisha ni nn ksha oa,, mtatoka tuu..
 
Dah yaani hio ni pesa ya Muuza Chips au Muosha magari ya siku moja! Au ya mhudumu wa Guest akishapiga Short time zake kadhaa. Hizi kazi za kuajiriwa eti kisa asubuhi unatoka umechomeka halafu unaenda kushinda kwenye kiyoyozi ni ujinga mtupu.

Kwa sasa tumia nafasi hio kufikiria issues nyingine kwa mfano, Loan na vitu ambavyo kazi ndio inakuaa Guarantor. Lakini baada ya hapo fuga hata kuku watakulipa kuliko hizi kazi, jana kulikua na thread hapa jamvini kuwa Ujasiri wako ndio Utajiri wako, kubali kuumia, kubali kuwa kuna nyakati biashara zako hazitakwenda vizuri lakini pia kubali kuwa kuna nyakati biashara zako zitashamiri sana.

Kwa mfano, ukinunua cherehani kimoja kila baada ya miezi miwili, ndani ya miezi sita utakua na vyerehani vitatu, kati ya hivyo fanya viwili ni vya kudarizia, jifunze kushona na designing, hizi course zinatolewa hadi VETA pale, baada ya hapo fungua ofisi yako ambayo kibanda kwa mwezi ni shilling 50,000 ukilipa kwa miezi sita ni laki tatu.

Baada ya hapo nunua vitenge, na viko, na mabatiki, shona hata nguo za viraka, tafuta mabinti wawili au vijana ambao watakupa support, hawa hutawalipa kwakua unawachukua kama Wanafunzi wako. kwahio unakua na labor ya kukusaidia kukata vitambaa, kuwatuma hapa na pale na kunyoosha nguo yaani finishing. Kwa sasa bei ya chini ya suruali ya kushona ni kama 25,000/= na shati sijui but una uhakika kila siku kurudi na shiling elfu tano minimum baada ya kukla na kufanya mambo yako mengine ambayo haina presha, haina NSSF, Haina Union sijui ya nini halafu ni Life Long Project.


hahahaahahahahaaaa ukija ukipata deal za kushona Uniform za CCM, Chadema, CUF, ACT, Masweta ya Wanafunzi, Sare za Mahoetili, Sare za kwenye Harusi na Send off, aaaghh lazima umshukuru MUNGU. Kubwa zaidi kwenye kazi kama hii ni kwamba haina kustaafu halafu hatimae unakua na vijana wengi ambao unakuwa wewe ndio msimamizi na kutafuta tender.

Mpwa hadi hapo unataka wazo gani tena? Thubutu, It can be done. natamani uifanye kitu kama hio uone jinsi hio laki sita utapita kwa muda gani, tatizo tunadharau sana kazi.

MUNGU akubariki sana
 
hyo nying sana mkuu lakin pia inategemea unafanya kazi wapi mim hua naenda kula hme coz ni karibu na wala situmii nauli
 
Ninafanya kazi Dar:

My gross salary: 610000;

Deduction is as follows:
NSSF (10%)= 61,000
PEYE = 65,700
HESLB (Education loan 8%) =48,800
CRDB loan=183,000

Worker union=12,200
BIMA YA AFYA = 10,800
Total deduction 381500
Net pay( take home) = 228500

228500 Ndio nauli, chakula, kodi ya nyumba na kila kitu dunia hii;
Nina miaka 31 lakini suala la kuoa halipo kabisa sababu ya kipato.

Mkuu vumilia hizo zenye red ujikwamue time will come utaenjoy tu, pia kwasasa angalia mbadala uongeze chanzo kingine cha mapato. Jiamini tu.
 
Elli
Pesa ya ,,,,ya siku moja? au ya short time����������
 
Last edited by a moderator:
Mpaka wakukate Tshs. 183,000/= huo mkopo ni mkubwa sana Na wote utakua ulikula bata mkuu pole sana huo mshahara ni mkubwa sana mzee tatizo ni Deni lako la CRDB
 
Acha kazi uone ilivyo ngumu kupata nyingine, tafuta source nyingine ya kukuingizia kipato kama miradi na biashara, naiman deni la HESLB na bank utaisha kipato kitaongezeka. Kikubwa kuwa mvumilivu punguza matumizi jibane maisha yatasonga.
 
Kwa mfano, ukinunua cherehani kimoja kila baada ya miezi miwili, ndani ya miezi sita utakua na vyerehani vitatu, kati ya hivyo fanya viwili ni vya kudarizia, jifunze kushona na designing, hizi course zinatolewa hadi VETA pale, baada ya hapo fungua ofisi yako ambayo kibanda kwa mwezi ni shilling 50,000 ukilipa kwa miezi sita ni laki tatu.


Mkuu mi sijaelewa hiyo hela ya kununua cherehani anaitoa wapi. Ada ya VETA anapata wapi? Hela ya kibanda kwa miezi mitatu anapata wapi?
Wakati huo anafanya kazi au kashaacha?
Lakin pia kumbuka kwa hali hii huyu mtu hasevu hata sh. 10.
Easier said ......
 
mkopo uliwekeza chini? Kwa makato hayo unaonekana ulipata mkopo wa kama milioni 6;ziko wapi?
 
kapumbiti kapumye
J.O.B = Just Over Broke.

Ss kwa kuelewa kurefu cha hpo usije ishi kwa kutegemea mshahara, kazi huwa ni sehemu tu ya kuanza kupata capital.

Kwa ushauri ukipata kazi,you are no. 1 -task ni kucreate businesss sio kuwork hard ili upate increments au bonus ukifanya hvyo utakuwa masikini milele na bepari wako atakuwa tajiri. kutafuta kazi ingine inaweza isiwe suruhisho bizness ndo suluhisho then kazi inakuwa ni sehemu tu ya reputation then ukikaa sawa hata hyo kazi unawaachia.

Kwa kuanzi huo mkopo uliouchukua ndo capital yenyewe ya biashara ss kama umeagiza passo uzwa mara moja...tafuta perfect business na acha kulalamika....Maisha ni kile ulichonacho kwa wakati huo usisubili ambacho huna. ambacho -huna kikujie wakati ukiwa tayali safarin.-

Hata mimi nilianza hvyo...sasa silalamiki tena...kilichopo kichwani ni kuacha kazi niendelee na biashara.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom