Natafuta Wataalam, Mlimao wangu ulipata Shida na majani kuanza kuwa meusi

kukumdogo

JF-Expert Member
Feb 1, 2011
2,866
2,746
Mlimao wangu ulipata Shida na majani kuanza kuwa meusi. Nilichukua Jani na kupeleka Kwa wataalam wanauza dawa za mimea wanajiita Mangito. Kufika palale kuwaonyesha na wakanipa dawa ya ukungu nikapulize. ILa kilichofuata baada ya kupuliza Ile dawa ni kuwa ilikuwa kama imewaboost na weusi kuzidi Hadi mlimao unashindwa kuzaa vizuri. JE hawa wataalam wapo kweli au ni kumaliziana hela Tu.
1644758307.jpg
 
Mlimao wangu ulipata Shida na majani kuanza kuwa meusi. Nilichukua Jani na kupeleka Kwa wataalam wanauza dawa za mimea wanajiita Mangito. Kufika palale kuwaonyesha na wakanipa dawa ya ukungu nikapulize. ILa kilichofuata baada ya kupuliza Ile dawa ni kuwa ilikuwa kama imewaboost na weusi kuzidi Hadi mlimao unashindwa kuzaa vizuri. JE hawa wataalam wapo kweli au ni kumaliziana hela Tu.View attachment 2883472
Hii ni sooty mold, ni fungus , unaweza kuspray mwarobaini(organic pesticide), madawa mengine ya fungus
 
Kimamba hiyo. Kama ni around nyumbani piga attakan c. Kama ni mbali na hauna maua piga sumu yenye profenofos zina harufu kali
 
tatizo sio ukungu ni wadudu. Hao wadudu ndiyo wanasababisha huo ukungu. Ukitibu ukungu ukaacha wadudu ambao ndo chanzo tatizo haliwezi kuisha
 
Na Mimi jamani mstafeli na mkokomanga yangu inazaa sana lakini wadudu wanaingia kwenye matunda, kwa hiyo matunda yote yanaoza. Msaada tafadhali
 
Na Mimi jamani mstafeli na mkokomanga yangu inazaa sana lakini wadudu wanaingia kwenye matunda, kwa hiyo matunda yote yanaoza. Msaada tafadhali
Nina changamoto hii pia. Ukijibiwa naomba unitag please..... Asante
 
Unatakiwa upulize dawa ya wadudu wakati wa maua, hao wadudu Huwa wanaacha mayai yao kwenye maua then tunda linapojitengeneza mayai yanajiangua, larva ndo waharibifu wanaweka matobo na vidonda hivo wanapunguza quality, spray insecticide wakati wa maua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom