Natafuta wa kunitengenezea Application za kwenye simu

Wanajamvi naomba kujua wap nawezapata watengenezaji wazuri wa application ya kwenye simu. Kma zle zilzopo playstor na gharama yke ni kma bei gan cjui.
Kama haujapata njoo pm tuongee kazi.
 
app ni very general term ni kama useme unataka kujenga nyumba kuna mafundi? Jibu ni ndio. Lakini nyumba zipo aina nyingi ambazo baadhi mafundi wengine hawawezi kujenga. Ukisema unajenga msonge utapata mafundi wengi na si ukisema ghorofa.

kwa hiyo maelezo yako hayatoshi kumfanya mtu hata avutike kufanya kazi yako. Kazi ambazo hazina maelezo mara nyingi huishia kusumbua maana mwenye kazi hajui anataka nini na hivyo kila "kizuri" akikiona anataka akiweke.

Nakushauri Ulipange wazo lako vizuri ujue unataka nini unaanzia wapi, unaishia wapi na bajeti yako. Then utakuwa umejua unahitaji wataalam wa aina gani na utakuwa na vigezo vya kuangalia.

Mwisho kuwa makini sana na vya dezo. Mara nyingi matapeli watakutajia bei very attractive na kukuacha kwenye mataa Bamaga ukishangaa. Hii ni kwa sababu akitapeli watu 10 kwa mwezi kila mmoja 500 000 huo ni mshahara wa 5M kwa mwezi. Lakini mtu serious na kazi lazima malipo yake yawe serious na kutegemeana na aina ya mobile app, epuka gharama zilizo chini ya 1M unless mhusika ni Mwanafunzi au anakaa kwa wazazi.

Kwa ushauri zaidi, wasiliana nasi (50, 000 per hour consultancy) tukusaidie kukushauri
0754 710 410 sisi ni Hosanna Higher Technologies (BRELA and TRA registered Company Based on Ubungo Riverside)
 
Back
Top Bottom