Bwana lutambi biashara ya hiace ni nzuri sana na wala si pasua kichwa kama watu wengi wanavyosema,upasua kichwa unakuja pale mtu anapoamua kununua hiace mbovu na baadaye anaanza kumsingizia dereva ..sina uhakika kwa 10ml utapata hiace nzuri,gari nzuri kwa biashara ni manual ambalo ni disel na bei yake ni juu kidogo,japo kuna watu wanatumia petrol ambayo ni automatic ambayo bei yake si juu sana,nilinunua hiace super roof dubai ya mwaka 2004 kwa $7500 ushuru wake ulikuwa ni 6ml baada ya hapo nililipia vibali vyote,toka siku hiyo napata hesabu tuliyoelewana na dereva hajawai kuniambia limeharibika au traffic amelishika..sasa mtu anataka gari cheap hajalipia vibali dereva akimwambia limeshikwa na traffic anasema dereva mbaya!!!nunua gari nzuri itakupa hesabu nzuri