Natafuta soko la ' unga wa ubuyu'

Natafuta soko la ' unga wa ubuyu'

Joined
Jun 20, 2013
Posts
13
Reaction score
1
Wadau nina bidhaa ya UNGA WA UBUYU, natafuta soko, ninao unga wa kutosha na bado naendelea kuuzalisha, mwenye kuhitaji awasiliane nami kwa namba zifuatazo 0712700280/0766550881. Napatikana Dodoma, karibu na Dodoma Hoteli ( Opposite Station ya Reli)
 
Acha kuzalisha mkuu huo si umepigwa marufuku na TFDA kua unasababidha kansa sa kwanini uendelee kuua watanzania wenzako
 
Unga wa Ubuyu ni BIDHAA??
kazi yake ni nini hasa?

Lima mahindi na maharage mkuu...achana na matunda pori.
 
wewe TFDA watakupigia watajifanya wateja halafu watahuharibu wote huo, bora unyamaze uuze kimya kimya, maana mamlaka ile siku hizi haieleweki, sijui wanafanya kazi kwa hisia? mara unafaa mara ni hatari kwa binadamu. ila soko lake kwa dar ni zuri sana.
 
hao tfda ni hivi ni watanzania kweli!!?
Haya mambo ya asilimia 10 cjui yataisha lini?
...eti unaleta kansa!!?hivi hyo kansa imeanza miaka hii?
Watz acheni ujinga!
Tunajua sana km hyo kitu imefanywa na hawa wenye bidhaa za kutoka nje ya nchi baada ya kuona zao haiuzi na watu,wakaamua kwenda huko kwa wakubwa ili kuharibu soko la ubuyu!
...hebu jiulize ubuyu umeanza kuliwa lini, na hakuna kemikali kinachoongezwa ss hyo kansa inatoka wapi?
na lini umefanyika huo utafiti kuwa unaleta kansa?
..wazungu wataendelea kuwatawala!
..pendeni vya kwenu!
 
Mdau kasema unga wa ubuyu sio mafuta ya ubuyu,

mafuta ya ubuyu ndio yamewekewa zengwe sio unga wa ubuyu

unga wa ubuyu unatumika kutengeneza icecream, juice , n.k
 
Acha kuzarau shughuli za watu tena za usiyemjua,

usije kuta mdau kakupiga gepu kubwa tu kimaisha na hayo hayo matunda pori,

unga wa ubuyu ni bidhaa??
Kazi yake ni nini hasa?

Lima mahindi na maharage mkuu...achana na matunda pori.
 
Back
Top Bottom