Natafuta soko la Sungura

Utapata soko mkuu, sema unahitaji maarifa na kutumia muda kutafuta soko sehemu mbalimbali hasa zilizoendelea katika mkoa wako, mfano katika maeneo ya mahoteli ya kitalii ama kawaida na migahawa mikubwa. Go direct uliza ama wape elimu kuhusu bidhaa yako watachukua.
Kama upo morogoro, naweza kusaidia kutafuta soko.
 
kuna kipindi sungura walihitajika sana na jamaa flani nadhani walikua outsiders, na walikuwa wananunua kwa bei nzuri sana, watu wakaingia mkenge na kufuga kwa kasi kumbe ilikuwa mpito tu.... pole ndugu, jaribu kwenda kwenye hizi hotel za kitalii mara nyingi menu zao na kitoweo cha sungura kinakuwepo.
 
Hotels ya kichina ipo kauda road wana agiza ila uwe na uwezo waku supplies 150 kila mwezi.. Ila kila asubuhi uwe unapeleka 5. Nenda kaogee nao
 
tatizo letu sisi wabongo porojo nyingi yaani unatafuta soko halafu unachouza huweki picha wala mawasiliano tuwaone,ninauhakika hapa hapa ungeweka picha na mawasiliano ungepata wateja hebu jaribu kujiongeza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom