Natafuta soko la mihogo

Natafuta soko la mihogo

Barackachess

Senior Member
Joined
Sep 1, 2018
Posts
158
Reaction score
123
Habari, Mimi nimelima mihogo, Ipo mlandizi sehemu moja inajulikana kwa jina la mzenga, ,Nimekosa soko, Naombeni mnisaidie ni wapi naweza pata soko, Nimelima heka 4 , Aina ya mihogo na mbegu ya mihogo inajulikana na MKIU. Nahitaji mawazo yenu hapa tu share kwa pamoja au kwa anae hitaji kununua.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huku Kigoma mihogo imeshuka bei, gunia la mhogo mkavu lililojaa na rumbesa tunauza 13-15,000/=
 
kwa jinsi bei ilivyoshuka huku mashambani, bora utafiti masokoni upeleke mzigo mwenyewe, pia jaribu kupeleleza soko la pale picha ya ndege Kibaha muhogo mwingi unaingia kutoka maeneo ya kisarawe
 
Kweli kuacha kazi kwa kutegemea kilimo cha kitanzania ni mtihani,na wachina wamekimbia na wanasiasa walioshawishi kilimo cha muhogo.mbaazi kg 150,nyanya ndoo kubwa 2000.Tujitafakari maana watu wamechapa ila hola.(Kuna Uzi jamaa anataka kuacha kazi akalime..nb.gunia LA mahindi 18000)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom