Natafuta sarafu ya Shilingi 20

Natafuta sarafu ya Shilingi 20

Weka bei hapa .Sio kitu cha ajabu duniani kuna watu huitwa coin collectors hununua coins kwa kuhifadhi au museum kama walivyo stamp.collectors Nilipokuwa mdogo nilikuwa na kialbum changu cha stamp za barua.Barua zikija nachana stamp nababdika kwenye kialbum kangu kikawa nazo nyingi za miaka tofauti tofauti .Kuna siku mzungu mmoja alikuja kijijini wa miradi ya elimu akanikuta na kakitabu kangu kenye stamp .Akaniuliza zaidi ya stamp unapenda nini? Nikasema napenda kuendesha baiskeli .Akaenda kununua baiskeli mpya akaniletea akasema tubadilishane yeye anapenda stamp minor stamp akawaambia wazazi wakampa akanipa baiskeli nzuri ya watoto baadaye iliniuma sana nikikumbuka stempu zangu nikaja gundua kuwa yule mzungu alikuwa au stamp collector au alienda kuuza kwa bei mbaya akaniachia baiskeli !!! Mleta mada weka bei watu tuchacharike chap chap kwa fursa
 
sarafu ya sh.20 ilitolewa na benk kuu ya mwaka 1961-1981 not otherwise na mimi ninazo izo uyo atakaekwambia ya mwaka tofauti na huu nilokupa kaa chonjo!
Rejea Historia vizuri bro sh.ishirini zipo pia kuanzia mwaka 90 kipindi cha utawala wa Ally Hassan mwinyii
 
Ni utapeli zipo za 1992
HUU utapeli umekaa jaaje, mtu anatapeliwa vipi? Mana naskia watu wengi wanasema ni utapeli.

Mimi ninazo sarafu zote zilizouliziwa, ni muda nazikusanyaga SIJUI ata sababu. Anayehitaji anicheki
 
Huu utapeli uliwahi mfirisi mshikaji wangu.

Yaani ni hivi huyu anaye nunua anazo hizo sarafu.atampatia mwenzake ajifanye anauza .kweli mara ya kwanza atanunua.halafu mara ya pili atakutangazia dau kubwa sana.halafu atokea mtu mwingine anazo hizo sarafu atajifanya anaziuza huyo naye atapandisha bei juu kidogo ila atakuwa nazo nyingi.ukishanunua tu,huyu jamaa atakwambia ameshaacha hiyo biashara.hivyo utabaki nazo mkononi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom