Natafuta rafiki wa kike atakayekuwa tayari kuolewa nami

ukuta2013

JF-Expert Member
Jun 16, 2013
275
98
Habari,

Mimi ni kijana wa kiume, nina umri miaka 30, Nina shahada ya kwanza, Nimeajiriwa (4 yrs now of experience) na nina kipato cha kawaida sana. Natafuta mchumba wa kumuoa ili siku moja awe mke wangu, rafiki yangu, mama watoto wangu and everything in my life. Naijua dunia na nimeamua kutulia (nafikiri naeleweka nikisema hivyo). Nataka kuanza safari mpya ya maisha yangu hapa duniani. Katika hili sitanii hata kidogo, Ubachelor nimeuchoka ni wakati wangu sasa na mimi kuanza maisha mapya ya ndoa, nipo serious sana katika hili.

SIFA ZANGU


Mimi ni mrefu 5.6", mweusi kiasi, sio mnene ila nina umbo kubwa, nina elimu ya wastani ya kupambanua mambo kiuchumi na kijamii, sijawahi kuoa, nina mtoto mmoja wa kiume (7yrs of age now), nimeajiriwa, najiendeleza kimasomo. Napenda kupendwa sipendi kutendwa. kwa hayo machache nitakuwa nimeeleweka au nimetoa picha kuwa mimi ni mtu wa aina gani.

SIFA
- Awe na umri kati ya miaka 25 hadi 28
- Awe muumini wa dini ya kiislam
- Awe na hofu ya mungu
- Awe tayari kupima VVU
- Awe tayari kuolewa ndani ya mwaka ujao (2014), mwezi, tarehe, na saa itategemea mipango tutakayokubaliana
- Awe tayari kulea mtoto wangu aliyezaliwa miaka saba iliyopita
- Awe mcheshi kiasi
- Awe mvumilivu kwa maana ya uvumilivu wa maisha kwa ujumla (Mabonde na Milima)
- Awe mkarimu
-Awe mpole wa wastani
-Awe na upendo kwa ndugu zangu ( nina kauli yangu moja kuwa "Mke wangu sio wangu peke yangu bali ni mke wa ngugu zangu, jamaa zangu, marafiki zangu na jamii nzima inayotuzunguka" kwa maana ya ukarimu wake kwao, heshima yake kwao, upendo wake kwao n.k) natumai nimeeleweka na ninaomba nisieleweke/nisinukuliwe vibaya/tofauti
- Awe na elimu ya kuanzia ngazi ya Diploma na kuendelea
- Awe ameajiriwa au kujiajiri
- Awe ni mtu anayeweza au mwenye utayari wa kutunza familia
- Awe na utu na asiwe mtu kitu
- Asiwe mchoyo (nafikiri naeleweka naomba nisinukuliwe vibaya)
- Na sifa nyinginezo zinazompasa mwanamke kuwa nazo ndani ya familia
Mwenye utayari na ambaye yupo serious ani-PM au ani-Email kupitia ukuta2013@gmail.com

NB: Please asiyekuwa tayari asome tu na apite, asitukane, asikejeli, wala asitanie kwani kufanya hivyo ni sawa na kuchezea hisia za watu/zangu.

Naomba kuwasilisha.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom