wala usisumbuke na midawa sijui nini,,, wewe kula ugali wa dona kwa maharagwe na nyama,, nilipofika hapa DRC haya mambo ya kuchangia nyumba na wazungu kila siku sijui lazanya sijui piza ,, wali nini ... nilikonda sana cha ajabu sasa mpishi yeye kitambi kinatoka tu siku moja nikapita jikoni ,,, masaleee nikakuta jamaa anafakamia ugali wa dona na ''sambaza; ikabidi niliweke wazi jambo hili pale office kha kumbe vitambi vyote pale ni sambaza kwa dona au ''kinono'' na siku moja moja ni ''kibonde'' vyooote lazima pembeni kuwe na ''sombe'' huwezi amini sasa nina kitambi namkaribia mwenda zake