Natafuta plot Arusha Njiro au Moshono

Natafuta plot Arusha Njiro au Moshono

Hute

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,537
Reaction score
6,479
Wakuu, natafuta kiwanja cha kujenga Arusha eneo la Njiro au Moshono, kisipungue nusu eka, eneo linalofikika lenye huduma zote, offer mkononi ninayo 30m. kwa atakayekuwa nacho, kinahitajika haraka, na unatakiwa kuweka specification za kiwanja hizo zote hapa na uweke na picha na mazingira yalivyo. pia, kiwanja kiwe kina hati (kwani nitapita ardhi kuserch), kama una mke au mume, hakikisha wanandoa wote mnaridhia kuuza na wote mtaingia kwenye mkataba na transfer ya ardhi. thanks.
 
Njoo maji ya chai nikupe kiwanja mzee baba
 
Kwa taarifa yako 30ml nusu heka huwezi pata kiwanja Njiro au Moshono. Njiro angalia uwe na 50ml. Nakushauri tafuta maeneo mengine kama kisongo. By the way Njiro na Moshono kuna shida ya upatikanaji wa maji sana
 
Mkuuu kwa ushauri wa harakaharaka Njiro sio sehemu salama kununua kiwanja kichwa kichwa utapigwa hiyo hela yako..nenda kwa uangalifu sana..kwa Arusha Njiro ni sehemu inayo migogoro mingi sana ya Ardhi..hivo kua makini..

NB: naongelea surveyed plots za njiro..
thanks, sehemu nzuri ni wapi mkuu. hasa ambako sio uswahilini...actually, nahamia arusha soon na sitaki nipange zaidi ya mwaka mmoja, hivyo nafika na kuanza kujenga ndo maana nataka kununua kiwanja soon after arrival. ila jueni mimi ni mwanasheria, najua due diligence ya kueleweka kabla ya kununua kitu hasa ardhi.
 
ni sehemu ipi arusha ukijenga ni sehemu ya middle class, at least hakuna uswahili, kila mtu anajua yake? please watu wa arusha nisaidieni.
 
ni sehemu ipi arusha ukijenga ni sehemu ya middle class, at least hakuna uswahili, kila mtu anajua yake? please watu wa arusha nisaidieni.
Moshono kuzuri, wellcome
 
wewe plots zimetangazwa mara kibao tu tena 12m tu ulikuwa wapi?!! tena ni hayo hayo maeneo ya moshono na njiro
 
wewe plots zimetangazwa mara kibao tu tena 12m tu ulikuwa wapi?!! tena ni hayo hayo maeneo ya moshono na njiro
ukisema nilikuwa wapi, utakuwa unanionea. jf kuna thread nyingi sana, na mtu kama hauna uhitaji wa kiwanja mji huo kwa wakati huo huwezi kuwa bothered na thread yeyote inahusu, na huwezi kutafuta. utaweza kusoma thread zote jf utaweza mkuu? sikuona mimi.
 
Nenda www.thesafaricity.com Matevez ni bonge la mji. Umeme upo maji yapo barabara za ndani zimechongwa na ulinzi upo. Barabara kubwa ya Afrika Mashariki kutoka Ngaramtoni hadi USA inapita ndani ya viwanja.

Viwanja vyote unapewa hati na sqmt 1=35,000. Nenda huko hutajutia pesa yako.
thanks mkuu kwa ushauri. huko nafikiri itabidi niwatembelee NHF kama sikosei. lakini hata huku mitaa mingine, kwenu ninyi wakazi wa arusha mkinipa ramani au picha walau sehemu zipi ni za kishua kuishi arusha, nitashukuru. thanks, God bless for your signature.
 
Safari City ndio kutakua USHUANI kuliko kwingine kote hapa Arusha. Mark my words na baada ya miaka michache utaniambia.

Ujenzi wake huhamishi udongo kama Kilala au Moshono. Ingawa kipenda roho hula nyama mbichi. Kama bado unapenda Moshono sawa ila ujue hakuna mitaa ni skwata!
 
.
Nenda www.thesafaricity.com Matevez ni bonge la mji. Umeme upo maji yapo barabara za ndani zimechongwa na ulinzi upo. Barabara kubwa ya Afrika Mashariki kutoka Ngaramtoni hadi USA inapita ndani ya viwanja.

Viwanja vyote unapewa hati na sqmt 1=35,000. Nenda huko hutajutia pesa yako.
Kwa nusu eka maanake ni 85m kama 1sqmt =35000
 
Safari City ndio kutakua USHUANI kuliko kwingine kote hapa Arusha. Mark my words na baada ya miaka michache utaniambia.

Ujenzi wake huhamishi udongo kama Kilala au Moshono. Ingawa kipenda roho hula nyama mbichi. Kama bado unapenda Moshono sawa ila ujue hakuna mitaa ni skwata!
wapi eneo sio skwata mkuu ili nitafute huko. please help!
 
ukisema nilikuwa wapi, utakuwa unanionea. jf kuna thread nyingi sana, na mtu kama hauna uhitaji wa kiwanja mji huo kwa wakati huo huwezi kuwa bothered na thread yeyote inahusu, na huwezi kutafuta. utaweza kusoma thread zote jf utaweza mkuu? sikuona mimi.
nssf kaloleni kwenye hiyo round about kulikuwa na bango daily lilikuwa linapigwa na vumbi likiwa na plots luluki sijui siku hizi limeishia wapi ila zilikuwa na bei fair sn
 
Back
Top Bottom