Natafuta nyumba ya kupanga tafadhali help me out

Umefanikiwa au ulikua unafanya utafiti? sijapata simu yako au kwa nini usiweke namba yako ya simu. Nisiseme sana pengine wakati unatafuta nyumba wakati huo huo unatafuta na kodi pia. Ndiyo maana watu wa Real Estate huwa watoza ada kidogo ili kama mtu anakuja kufanya utafiti asiondoke hivi hivi bila kuacha kitu kidogo. Karibu.
 
Unatafauta nyumba ya kupanga, wewe uko wapi na unataka nyumba wapi....tanga , mwanza, songea au masasi? Be specific my friend usaidiwe
 
Natafuta nyumba ya kupanga vyumba viwili maeneo Kimara,ubungo,mbezi,kijitonyama,mwenge.....kodi TSH300,000-TSH400,000,ikipungua ndio furaha yangu.

Tafadhali mwenye maujuzi haya nisaidie.

Natanguliza shukrani zangu.




Mji una nyumba yenye vyumba viwil vya kulala, moja kati ya hizo ni self contained (ina choo ndani)Ina sebule, dining room, jiko na public toilet iliyotenganishwa na bafu. Pia ina nyumba nyingine ya biashara yenye frame mbili za duka, chumba cha kulala, veranda kubwa mbele na choo cha nje. Mji wote uko ndani ya eneo la wazi la nusu heka na eneo lote lina fence na gate. Inafikika kwa gari, ina mfumo wa maji ya bomba pamoja na tank la chini ya ardhi yenye uwezo wa kuhifadhi lita 10,0000. Kuna umeme wa Luku. Nyumba ni ya vigae na ina finishing ya kisasa ya tiles (Spanish ceremic tiles)na gypsum ceiling.
Bei ya kupanga mji wote-yaani nyumba kubwa pamoja na frame za biashara+chumba cha nje ni Tsh. 200,000 (Laki mbili tu) kwa mwezi. Malipo ni kwa mkupuo wa miezi 12. Nyumba iko Changanyikeni Mbuyuni-karibu sana na HOSTEL ya Jesus Village. Ni umbali wa kutembea kwa miguu kwenda chuo kikuu (Mlimani), mlimani city, Chuo cha Ardhi na Chuo cha Takwimu. BAADHI YA PHOTO ZIMEAMBATANISHWA
Kwa mawasiliano zaidi tafadhali piga simu numba 0714554390 au email:daktarimicha@yahoo.com

Asanteni


Attached: DSCF0529.JPG (1,000.3 KB) DSCF0513.JPG (1.28 MB) DSCF0521.JPG (1.48 MB)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom