Natafuta Nyau wa Kula Panya

Ramthods

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
515
186
Wadau,

Hivi karibuni nimekubwa na usumbufu wa panya. Wanatoboa madirisha na kuingia ndani nyakati za usiku. Nimejitahidi kupambana, ila nimeona paka atakuwa suluhisho la kuaminika. Nikiweka sumu wanafia kwenye kona, wanaozea huko!

Sumu nyingine nadhani ni feki, wakila hawafi!

Nani mdau mwenye paka mdogo, lakini mwenye uwezo wa kuwatimua hawa wabwana mbio anipe tafu kabla sijanunua sofa mpya?

Nipo Dar, mitaa ya Mbezi beach!

Natanguliza shukrani!
 
ni kwa nini panya wanakuwa wengi kwako...unafuga kuku?....
 
Ninakaa Mbezi Beach tangi bovu, paka wangu amezaa kama mwezi mmoja uliopita ana watoto watatu. Lakini naondoka kesho kwenda Zanzibar kwenye vakesheni kidogo na famili. Kama tatizo lako ni paka mdogo kweli, just PM me... will be back on Monday
 
Mkuu, naona umenipa mwangaza!

Kuna kuku wa kienyeji upande wa nyuma, kama kumi hivi!

Embu niambie, kuna uhusiano gani kati ya kuku na panya? Ukweli haikuwa hivi kipindi cha nyuma, na inawezekana wameanza kipindi hawa kuku tumeanza kufuga!
 
Shukrani mkuu,

Ntakucheki kesho, mida hii naona ni late sana.

I can wait until monday, no problem!
 
Mkuu, naona umenipa mwangaza!

Kuna kuku wa kienyeji upande wa nyuma, kama kumi hivi!

Embu niambie, kuna uhusiano gani kati ya kuku na panya? Ukweli haikuwa hivi kipindi cha nyuma, na inawezekana wameanza kipindi hawa kuku tumeanza kufuga!

yah....kuna kahusiano ka kuku na panya.......nadhani uhusiano wao mkubwa unasababishwa na ile pumba wanayokula kuku......dawa hapo ni kuhamisha hao kuku karibu na nyumba au kuwamalizia kwenye sufuria
 
au ni enzi za Farao na wana wa Israeli ndizo zimeanza kurudi? Si unakumbuka yale mapigo? ndio yameanzi mitaa ya kwako
 
Makoyo, hahahahahah hivi unawaza nn? hahahahahah you mada my night, naenda kulala sasa hahahahahahahah!!! LOL
 
ukipata paka usimlee kama yai hatafanya kitu

Your 100% ryt, ukimlisha sana huyo paka hatakuwa na mda wa kufukuza panya badala yake analala tuu na kunenepeana, mshindishe njaa atakuwa active kuwinda panya. Kama ni paka jike kamtoe kizazi ili asijepata mimba na kushindwa shughuli uliomletea ya kufukuza panya.
 
species ya nyau wanaokula panya imepungua sana siku hizi. Sijui ni mabadiliko ya hali ya hewa ya dunia.teh teh teh

Zamani hata mbwa na paka walikuwa maadui

Usiwe mkatili wa kutaka kuwauwa . kwenye chakula chao wawekee vidonge vya kutozaa. Nenda kwa ma vet watakupa .ust consider them as pet.

Teh teh teh
 
Wadau,

Hivi karibuni nimekubwa na usumbufu wa panya. Wanatoboa madirisha na kuingia ndani nyakati za usiku. Nimejitahidi kupambana, ila nimeona paka atakuwa suluhisho la kuaminika. Nikiweka sumu wanafia kwenye kona, wanaozea huko!

Sumu nyingine nadhani ni feki, wakila hawafi!

Nani mdau mwenye paka mdogo, lakini mwenye uwezo wa kuwatimua hawa wabwana mbio anipe tafu kabla sijanunua sofa mpya?

Nipo Dar, mitaa ya Mbezi beach!

Natanguliza shukrani!

Hilo la paka ni wazo zuri sana,jitahidi kuwasiliana na aliyekupa offer ya kanyau kadogo lakini ufuate masharti ya ufugaji wa nyau asijekuwa nyau koko tu.Na hapo nilipo hi light ni vizuri wakati unanunua sumu hiyo uhakikishe kama ni feki au sio feki kwa kuionja kidogo maana hizi bidhaa za kichina siku hizi zimeharibu sana ubora wa bidhaa.
 
mhh huu ushauri huu,umekaa kinec huu
 
Pole sana mkuu. kuna msemo kwamba panya woote wa ndani ya nyumba ni mali ya baba.
Hapo kwenye bold nataka nikushauri kwamba, punguza mazagazaga yasiyo na maana ndani ya nyumba. hakikisha viti, kabati, vitanda vinaacha nafasi ya mtu kupita nyuma yake.
Kitu kingine kuhusu panya, jitahidi kuweka eneo linalozunguka nyumba ktk hali ya usafi. choma taka ama chimba shimo uziweke humo, fyeka majani au vichaka, kama kuna rundo la items zipange vyema ili kuondoa uwezekano wa panya kujenga makazi au kujificha humo.
Nakwambia hivyo maana siku hizi panya na paka are friends utashangaa unafuga paka anaishia kula samaki na maziwa na hali panya mpaka akamatiwe na kupikiwa.
 
ni kwa nini panya wanakuwa wengi kwako...unafuga kuku?....
PRETA, ukiona kuna panya ndani ya nyumba ujue kuwa nyumba hiyo ina neema yaani hawalali njaa na hawali mlo mmoja. Kukosekana panya ndani ya nyumba ni dalili kwamba ninyi ni mabahili na njaa kali
 
yah....kuna kahusiano ka kuku na panya.......nadhani uhusiano wao mkubwa unasababishwa na ile pumba wanayokula kuku......dawa hapo ni kuhamisha hao kuku karibu na nyumba au kuwamalizia kwenye sufuria
Nashukuru sijakuoa maana ungenitia kwenye lindi la ufukara weye binti hahahahahaha
 
jamani jamani...bila kufanya hivyo hao panya si watatutafuna na sisi...mwee...bora kudestroy hao kuku....ha ha ha....Happy New Year
 
Kweli we paka mweusi akili zako hazina akili. Umenifanya nicheke kicheko cha kuanzia mwaka.

Unamshauri mwenzio aonje kidogo sumu?

Haya we pusi

Hilo la paka ni wazo zuri sana,jitahidi kuwasiliana na aliyekupa offer ya kanyau kadogo lakini ufuate masharti ya ufugaji wa nyau asijekuwa nyau koko tu.Na hapo nilipo hi light ni vizuri wakati unanunua sumu hiyo uhakikishe kama ni feki au sio feki kwa kuionja kidogo maana hizi bidhaa za kichina siku hizi zimeharibu sana ubora wa bidhaa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom