Natafuta nguo za watoto kama hizi

Natafuta nguo za watoto kama hizi

Raimundo

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2009
Posts
13,415
Reaction score
12,628
Natafuta nguo za Ben 10 kama hizo zinazoonekana kwenye picha, duka gani naweza kupata hapa Dar? Mwanangu ana birthday na ningependa apige moja wapo ya hizo pamba.

Msaada wadau.


View attachment 184492


 
Naskia Ben ten ni free mason! Angalia watoto wako wasije wakatajirika fasta wakakuzidi kipato... Teh teh. Happy birthday to your kid...
 
hizo picha umezitoa wapi? hapo ulipozitoa ndiyo sehem nzuri ya kununua kwa bei nzuri.
 
halafu hii mambo ya Ben Ten muichunguze vizuri.
kwa watoto si nzuri sana.
Angalizo. Mwenye macho na asikie.
 
Ni sheeeeeeddddaaaa.
ben10-wallpaper-14.jpg
 
Pamba kali,hata mie nimezipenda.

Ben 10 haina tatizo.
Hivi tujiulize hawa freemason wapo zaidi ya karne,sasa imekuwaje kuanzia miaka ya 2008 ndio mambo yaanze kuvuma hapa nchini,hasa kwa vijana?
Hizi ni fikra potofu sana,na wengi waliozikazania ni wale wenye roho mbaya na maisha ya wenzao wanaojituma kutafuta na wakitumia pesa zao vizuri kwa nidham.
Wapo watu tunawaona kabisa kwamba wanafanyakazi kwa bidiii kupata pesa,unasikia mtu anakurupuka hao ni freemason,wakati huohuo unajua kabisa kwamba kasotea sana kuhangaikia pesa wakati huo wewe ukila bata bila malengo.
Na hii siku hizi hadi watoto wadogo utawasikia Freemason,ni hatari sana kwa kizazi chetu,yaani hadi watoto wanakuwa na fikra kwamba huwezi kufanikiwa kimaisha ila utakuwa ni freemason.
Fanyakazi,weka nidham ya pesa,weka malengo ya muda mfupi na muda mrefu,fanya ibada sana kwa imani yako,fanya maombi sana kwa imani yako,kisha mkabidhi mungu atajua lini au mwaka gani atakuwekea mambo yako sawa,kwakuwa mungu anaona juhudi na anajua malengo ya kila mmoja kwamba akimpa pesa au mali atafanya nini na atamfanyia nini Mungu kiimani.Hapo wengi tunakwama kwenye anasa tu,na muda mungu akichukua fungu lake ili ujifunze ndio kwanza haoo tunakimbilia kwa waganga.

Tujipange vijana,tuache mitizamo isiyo na tija.
Dunia ya sasa kila kukicha watu wanakuja na mitizamo yao ya kishetani na kutoka nje ya imani zao za dini,juzi tu mtu kazuka na kusema Pombe ni dawa ya ukimwi,Kibwetere nae aliwauwa watu kwa imani hizohizo,na ipo siku atazuka mtu na kusema ukijisaidi haja kubwa ndani ya nyumba ni mkosi mkubwa sana,hapo inabidi watu tuingie mwituni kama zamani au kuachia kubwa kwenye eneo la jirani.

Tupitie Maandiko,sio kwenda nyumba za ibada tu kama vile unaenda Picnic,yapo mengi ya kujifunza na kila kitu kipo wazi sana.Mungu ni Mwema sana.
Tubarikiwe sote
 
Back
Top Bottom