Hili ndio linalosukuma wanaume wengi wasiokuwa na watoto kwenye ndoa kuzaa nje ya ndoa. Maana ukishazeeka utaambiwa hata wa kusingiziwa huna?? Basi ulikuwa na matatizo wewe. Sasa ili kuepuka hayo nawashauri wanaume wenye shida hii wachukue hatua mapema..
HIVI UKIWA NA MIKA SABA BILA HATA MTOTO. NA UKAGUNDUA SHIDA IPO KWA MWANAMKE. WEWE KAMA GREAT THINKER UTASHAURI MWANAUME ACHUKUE HATUA GANI???. tUSIONGEE TU KUFURAHISHA JAMIII. JE MUME AKUBALI KUISHI MAISHA YAKE YOTE BILA MTOTO???
Lakini huyu tayari ana mtoto
MkimbizwaMbio huyu mtu ana watoto wawili tayari wa mke na wa kwake sasa anachotafuta huko nje ni nini kama sio uzinzi tu? Mkewe angekua hajawahi kumzalia mtoto sawa lakini ameshazalia mmoja na anamwingine pia aliemzaa ujanani so mke ana mayai ya kutosha tu, pengine huyu baba ndio alikua na yai moja mbona hana hata wa kusingiziwa huko nje? Hana shida ya mtoto huyu anatafuta mwanamke wa kuzini nae tu
Wewe unaonekana ni sizitaki mbichi hizi, sababu huna sifa. Nimecheki email yangu sasa hivi, tayari kuna mademu 3 wameishatuma contact. Maty wanawake wa kuzini nao tu sio wa kuangaika kutafuta. Wako kibao hata ukitaka kumi kwa siku unawezakupata. Naona we hauko kwenye viwango ndo maana unapiga filimbi sana. Wewe usitake nifanye unachotaka wewe. Badala ya kutoa ushauri wa maana kumsaidia mtu wewe unapuliza filimbi tu.
Sawa baba mie sizitaki mbichi hizi natamani kuzaa na wewe ila sina vigezo hayo ni mawazo yako na umewaza vyema.
Ila ni hivi hao wanawake waliokutumia email ni vilaza kama wewe nachelea hata huyo mtoto utakaezaa na mmoja wao atakua kilaza pia. Mwanamke mwenye akili timamu angemfikiria huyo mkeo kwanza atajisikiaje akisikia mumewe aliekaa nae miaka yote hiyo ameenda kuzaa nje kisiri angekua yeye angefurahia hayo
pili angewaza kwa nini azae mtoto ambae wewe unataka iwe siri ajekujulikana siku ambayo we utakufa labda ndio ajitokeze eti alizaa na wewe
tatu labda huyo mwanamke angekua mbaya kama mimi na hana elimu kama mimi nilieishia std IV na mama wa nyumbani kama mimi ningemuelewa. Lakini mwanamke mrembo na kajiform six kake na kazi yake na ofcourse huwezi kuwa na kazi kama umeishia form six lazima ana kajidiploma au kadegree (hiyo form six yako pekee haiwezi kumpatia mtu kazi) anakubaliana na matakwa yako inaonyesha hakuna wanaume ambao hawajaoa waliomtamani miaka yote hiyo lazima ana matatizo makubwa ndio maana anakubaliana na ujinga wako
Hivi hapo nimetumia lugha ya matusi ee
upo sahihi kabisa! LikeMmmh anayetaka kuzaa nje hatangazi........
Hakuna kitu humo. Ungekuwa una kitu ndani ungeniuliza maswali ya msingi kwanza nami nikakujibu ndo ungepata ku-draw conclusion ya maana. ungeuliza ni kwa nini nataka mtu mwenye sifa nilizotaja labda, uhuru wa mtoto kwenye familia yako utakuwaje, huo usiri wa kuwa na mtoto wa nje utakuwa wa muda gani, nk. Unakurupuka tu na kujifanya unajua mipango na mawazo yangu yote. Think out of box. Kama wewe umelemewa na matatizo ya maisha, tafuta msaada, mbinu na ushauri kwa watu. Sio kuleta hasira za kukosa mwelekeo wa maisha hapa.