Natafuta Mwanamama ili awe rafiki yangu 'mzurimzuri'

funluverx

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
480
342
Umri usiozidi miaka 35.
Awe mtanzania wa kuzaliwa.
Asiwe amewahi kuwa ndani ya Ndoa (Kuolewa na kuachika-Hapana)
Awe amesoma angalau kiasi.
Awe mwenye Hofu ya Mungu.
Awe anajitambua na mwenye kujishughulisha.
Mvuto wa ndani uushinde mvuto wa nje.
Akiwa na Ajira yake/Kazi yake itapendeza ila si lazima.
Awe anaishi Tanzania au Nje ya Tanzania lakini Uraia shurti uwe wa Tanzania.

Nia na madhumuni ni urafiki ambao utaelekea mbele zaidi iwapo tutaridhiana,kuendana na nafsi zetu kukubaliana.

Mimi nina uraia wa Tanzania,
Muislam na mwenye Umri wa Miaka 40,
Sikuwahi kuwa kwenye Ndoa,
Nimejiajiri na nina kipato cha 'Mkononi kwenda Kinywani'.

Mwanamama sikiliza nafsi yako na chukua maamuzi sasa iwapo unazo sifa tajwa.
Sifanyi mas'khara hapa.

Ukiwa unaye rafiki mwenye sifa hizo unaweza kumfahamisha pia.

Tuma maelezo yako binafsi PM.
 
Ww ni mvulana uliofikia umri wa miaka40 Dini ya kislam. tena hujawahi kuoa. Na jaribu kuwaza watoto ulionao yote wanagharamu. Na bado unatangaza unataka urafiki mwingine . Je kumrudia mungu wako ni lini? Na hadi kumuomba istighfara kwa yale ulioyatenda? Nakushauri usituchafulie imani yetu...
 
Subhanaallah..... Haya sema shekh kachafuaje Iman yetu? Usishangae ukamkuta firdaus huyu!
 
Sijaandika mahali kuwa mimi ni mvulana.
Miaka 40 ndio, Shida nini?

Kuna gharama? ipi na inakuhusuje wewe?
Yangu mimi na Mungu-wangu yananihusu mimi na Mungu wangu, si wewe tulia tuli.
Si Haki,wajibu wala Kazi yako kunihukumu.

Unauhakika gani kuwa namuasi Mungu hadi useme nimrudie,
Kwa dhambi gani ulioishuhudia nikiifanya?

Kutafuta Mke kwa Nia njema ndio kuuharibu Uislam?

Yaekelea wewe ni Muislam kupita Uislam wenyewe.
Lakini naomba uniache tu, Kama dhambi yangu mie, sawa Shekhe?
 
kila la kheri mkuu na ukimpata tafadhali uje na shukrani tele kwa JF
 
Subhanaallah..... Haya sema shekh kachafuaje Iman yetu? Usishangae ukamkuta firdaus huyu!
Waafrika tuna matatizo sana kwenye Imani.

Ila kwasababu anajua sana wala sitabishana nae maana hawa ndio akihifadhi Juzuu Amma Tu anaona wenzake wote hawaendi Peponi isipokuwa wao.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom