Natafuta mtu makini wa kushirikiana na mimi kuwekeza katika kilimo

Mkulima2002

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
291
211
Salaam Wakuu,
Mimi ni kijana muhitimu wa Chuo kikuu. Katika mapambano ya kusaka mkate wa kila siku nimeona ni vema nikajikita katika kujiajiri. Naaam kujiajiri katika sekta ya Kilimo na ufugaji, sasa nimeona ni vema nimtafute kijana/vijana mwenzangu tuunganishe nguvu na tufanye kitu kimoja chenye kutuletea kipato halali.
Karibuni wadau.
 
umeulizwa unatazamia kulima nini hujibu, umeulizwa upo wapi hujibu. acha utani tafadhali nimeshindwa kuuliza hata swali langu sababu ya kwanza hujajibu
 
Unatazamia kuwekeza kwenye kilimo cha mazao gani??
Niwie radhi kwa kuchelewa kujibu..
Uwekezaji huu utatarajia na makubaliano yetu kati ya Mimi na nitakaye kuwa nae.. Infact ninapenda sana kuwekeza katika zao la mihogo ingawa hapa lazima tujihakikishie soko wizarani kwani ni hivi juzi tuu wizara hasa ya viwanda chini ya Mh Mwijage ilisema China imefungua soko la mihogo tank million 300..
 
umeulizwa unatazamia kulima nini hujibu, umeulizwa upo wapi hujibu. acha utani tafadhali nimeshindwa kuuliza hata swali langu sababu ya kwanza hujajibu
Niwie radhi mkuu kwa kuchelewa kujibu. Nimeshatoa majibu kwa wadau wote hapo juu..
Karibu kwa swali ama wazo
 
Niwie radhi kwa kuchelewa kujibu..
Uwekezaji huu utatarajia na makubaliano yetu kati ya Mimi na nitakaye kuwa nae.. Infact ninapenda sana kuwekeza katika zao la mihogo ingawa hapa lazima tujihakikishie soko wizarani kwani ni hivi juzi tuu wizara hasa ya viwanda chini ya Mh Mwijage ilisema China imefungua soko la mihogo tank million 300..
Na kuhusu muhogo ambao unatoa mazao mengi, unaweza kuwasiliana na Dr Mkamilo wa Kituo cha Utafiti (Agricultural Research Institute ARI -Naliendele) kule Mtwara. Hao ni wataalam na watakushauri jinsi ya kulima kisasa zaidi na kupata mara nne zaidi ya kilimo cha kawaida kwa hekari moja.

Ni wazo zuri, kule Rufiji kuna ardhi nzuri kwa kilimo cha Muhogo. Natamani nikujoin kwenye hicho kilimo
 
Kweli kaka

Kweli kaka hata nilipokuwa nafanya uchunguzi wengi walinishauri mbegu lazima niende Naliendele kwa mbegu bora sana.. Asante kwa jina la Dk kwa ajili ya mbegu.. Lkn pia njoo kaka tuwekeze kaka huku kuna utajiri sana mkuu wangu
 
Poa ndugu Mokoloko nitafanya hivyo punde.
kwanza niombe samahi kama nitakua nimeatoka nje ya mada,
ila mimi vijana ninatafuta mashamba ya kulima ambayo yapo pembezoni mwa jiji la dar es salaam,sio ya kukodi ila kununua.
Kweli kaka

Kweli kaka hata nilipokuwa nafanya uchunguzi wengi walinishauri mbegu lazima niende Naliendele kwa mbegu bora sana.. Asante kwa jina la Dk kwa ajili ya mbegu.. Lkn pia njoo kaka tuwekeze kaka huku kuna utajiri sana mkuu wangu
Kweli kaka

Kweli kaka hata nilipokuwa nafanya uchunguzi wengi walinishauri mbegu lazima niende Naliendele kwa mbegu bora sana.. Asante kwa jina la Dk kwa ajili ya mbegu.. Lkn pia njoo kaka tuwekeze kaka huku kuna utajiri sana mkuu wangu[/QUOTE
 
Salaam Wakuu,
Mimi ni kijana muhitimu wa Chuo kikuu. Katika mapambano ya kusaka mkate wa kila siku nimeona ni vema nikajikita katika kujiajiri. Naaam kujiajiri katika sekta ya Kilimo na ufugaji, sasa nimeona ni vema nimtafute kijana/vijana mwenzangu tuunganishe nguvu na tufanye kitu kimoja chenye kutuletea kipato halali.
Karibuni wadau.

Mkuu, naunga hoja! Mimi ni muajiriwa hapa morogoro, nina eneo la heka 13 katika kijiji cha ruwe, kata ya Mafuru, wilaya ya mvomero, huko ni nje ya mji. Ningependa kuungana nanyi kwa kuwakaribisha kufanya kilimo hicho kwenye hili eneo maana muda huu nimebanwa sana hivyo nashindwa kupaendeleza ipasavyo.
 
Asante sana kaka, sasa naomba tupange jinsi ya kuonana nawe kaka, naweza hata kusafiri kuja kipande hiyo. Naomba mrejesho kaka.
 
kwanza niombe samahi kama nitakua nimeatoka nje ya mada,
ila mimi vijana ninatafuta mashamba ya kulima ambayo yapo pembezoni mwa jiji la dar es salaam,sio ya kukodi ila kununua.
Poa kaka, lkn kwa nje ya DSM yapo ila ninawasiwasi na bei ikawa changamoto(samahani kwa kuusemea mfuko wako) ila nitarudi hapa kukuletea namba ya mtu wa kukutaftia
 
Back
Top Bottom