Natafuta msichana wa kuuza Stationery

magode

JF-Expert Member
Oct 2, 2014
2,204
3,337
Wanajamvi,
Amani kwenu..!

Natafuta msichana wa kuuza duka la vifaa vya maofisini,shuleni nk.

Sifa;
-Elimu angalau kidato cha nne.
-Awe anajua kutumia computer
-Asiwe ameolewa.
-Awe anaishi kinondoni(duka lipo kinondoni).

Mshahara ni laki moja na nusu kwa mwezi. Atapewa chai na chakula cha mchana.

Kufungua ni saa 2 asubuhi mpaka saa 2 usiku. Jumatatu mpaka jumapili.

Atapumzika siku moja ktk juma,hiyo atachagua mwenyewe apumzike siku gani.
Mwenye kuhitaji ani-pm.

Nawasilisha.
 
MKUU..
TAYARI NIMEKUTAFTIA WAPO KAMA WANNE..

SO UNAWEZA KUCHAGUA.

WAKWANZA NI +255764204154
 
nashindwa kuja pm kwa mfumo huu mpya, bt nipo kinondoni naweza iyo kazi au umeshapata mtu tayar?
Sijapata mtu,nakuwekea mimi mawasiliano yangu pm utanicheck au huwezi hata kusoma pm???
 
Wanajamvi,
Amani kwenu..!

Natafuta msichana wa kuuza duka la vifaa vya maofisini,shuleni nk.

Sifa;
-Elimu angalau kidato cha nne.
-Awe anajua kutumia computer
-Asiwe ameolewa.
-Awe anaishi kinondoni(duka lipo kinondoni).

Mshahara ni laki moja na nusu kwa mwezi. Atapewa chai na chakula cha mchana.

Kufungua ni saa 2 asubuhi mpaka saa 2 usiku. Jumatatu mpaka jumapili.

Atapumzika siku moja ktk juma,hiyo atachagua mwenyewe apumzike siku gani.
Mwenye kuhitaji ani-pm.

Nawasilisha.

Mkuu mbona unahitaji wasioolewa tu? Kuna shida gani?
 
Mkuu mbona unahitaji wasioolewa tu? Kuna shida gani?
Ni kwa sababu ya muda,anatakiwa kufungua saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku. Kwa aliyeolewa ni ngumu kutokana na majukumu ya kifamilia. Ndo maana pia nataka awe anatoka kinondoni karibu na ilipo ofisi.
 
Ni kwa sababu ya muda,anatakiwa kufungua saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku. Kwa aliyeolewa ni ngumu kutokana na majukumu ya kifamilia. Ndo maana pia nataka awe anatoka kinondoni karibu na ilipo ofisi.

Mkuu unazijua sheria za kazi?
Kama huzijui nakushauri ufuatilie na uzifahamu vyema. Maana huyo binti atakuwa anafanya kazi zaidi ya masaa 12 kwa siku, kwa siku 6 ktk wk
 
Back
Top Bottom