Natafuta Mkopo

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,206
18,548
1.Natafuta kampuni inayo toa mkopo hadi mil 10
2. Natafuta kampuni inayo toa mkopo wa bidhaa kama bajaji, Kirikuu , au magari aina ya Noah

Naomba atoe vigezo na masharti ya mkopo.
asante
 
nenda kwenye taasisi za kifedha na wala si hapa nenda UTT, POSTA BENK , EQUITY wanatoa mpaka na pikipiki na mashine
 
mfanya biashara

kama hivo njia nyeupe mkuu jitahidi nenda akiba na access bank watakuelekeza ufanyaje mradi biashara yako inaweza lipa na unajua input yake huku ukiwa na vibali vyote fasta unapata sikushauri hizi taasisi watakuumiza maana mkopo unapewa wa muda mfupi bank ukimba almost two years
 
Kimuonekano inaonekana unajaribu kuingia kwenye biashara.Nakushauri kwa mara ya mwanzo bora usubiria miaka kumi ili upate pesa yako.
Ila mkopo wa gari ni hatari tena hatari saana tofauti na unavyodhania.

Mie namiliki hivyo virukuu unavyosema,na bodaboda,na nilianza na moja mpaka leo na kadhaa,sidaiwi na mtu na sikuchukua mkopo kwa mtu,ila changamoto naziona,na huwa najiuliza je ningekuwa na mkopo bank sijui hali ingekuwaje.

Maana magari yote uliyoodhoresha ni kwamba una target kuyatia kwenye biashara,umevyotaja tu aina nimejua unaelekea wapi.
Ni bora uanze na chako kimoja then ndio uingie kwenye mikopo.Unaweza kukuta uharaka wa maisha unakuja kukufanya hata ulichokuwa nacho kuchukuliwe.
 
Wabongo waoga sana kukopa. Jamani ili tujikwamue na umasikini ni lazima tukope km hatuna mjomba,kaka au dada Wa kukupa mtaji na ukikopa kwa ajili ya kuiendeleza biashara jitahidi hiyo pesa uifanyie biashara kweli ukibadili matumizi tu inakula kwako
 
ve
Kimuonekano inaonekana unajaribu kuingia kwenye biashara.Nakushauri kwa mara ya mwanzo bora usubiria miaka kumi ili upate pesa yako.
Ila mkopo wa gari ni hatari tena hatari saana tofauti na unavyodhania.

Mie namiliki hivyo virukuu unavyosema,na bodaboda,na nilianza na moja mpaka leo na kadhaa,sidaiwi na mtu na sikuchukua mkopo kwa mtu,ila changamoto naziona,na huwa najiuliza je ningekuwa na mkopo bank sijui hali ingekuwaje.

Maana magari yote uliyoodhoresha ni kwamba una target kuyatia kwenye biashara,umevyotaja tu aina nimejua unaelekea wapi.
Ni bora uanze na chako kimoja then ndio uingie kwenye mikopo.Unaweza kukuta uharaka wa maisha unakuja kukufanya hata ulichokuwa nacho kuchukuliwe.

very well put mkuu

yani watu wasionavyo barabarani wanaona wenye navyo yani kila siku ni mtelezo..wakati kuna siku pasua kichwa mpaka unawaza waweke parking magari yote na viboda boda vyote
 
Back
Top Bottom