Natafuta mke wa kufunga nae ndoa

Natafuta mke wa kufunga nae ndoa

MwanaSaikolojia

Senior Member
Joined
Jan 9, 2015
Posts
197
Reaction score
62
Mimi ni kijana wa umri miaka 25 nina cheti cha form 4,nimepanga chumba Usagara kwa sasa sina ajira nipo nasaidiwa na ndugu zangu nahitaji mke ambae tayari anayo kazi ili tuweze saidiana majukumu.

Asiwe mnene sana wala asiwe mfupi sana, awe msafi pia yule ambae ni bikra atakua na nafasi nzuri zaidi ya kuwa mwenza wangu wa maisha.

Awe angalau ana diploma na umri kati ya 23-26 kwa anae hitaji anifate inbox mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 5 mwezi huu.

Asanteni sana
 
wewe umevurugwa, mkuu pesa huna masharti mpaka bikra unataka? na bakhresa atake nini? afu unaweka na deadline?duh.
 
wewe umevurugwa, mkuu pesa huna masharti mpaka bikra unataka? na bakhresa atake nini? afu unaweka na deadline?duh.

Hamna mkuu hujanielewa.. yaani nmemaanisha bikra itakua kama credit vile.. kwa mfano wakigombea 10 sasa yule ambae ni bikra ndie ntaemuoa.. na pesa haina mwenywe naamini ipo cku tu na mie ntaipata
 
umenichekesha vitu vifuatavyo.
1: kazi huna
2: pesa huna
3: elimu form four halafu unataka
mwanamke wa diploma,
4: pesa huna halafu unataka bikra
5:unataka mwanamke mtumishi wakati
wewe huna ajira.
tafuta ela kwanza lakini ni ushauri wangu huo kwako , acha kuishi kwa matumaini kwamba utapata ela mbeleni anza kuhangaika sasa .
 
Eti hii thread nayo imekuwa sponsored na Tecno.. dah
 

Attachments

  • 1425269729132.jpg
    1425269729132.jpg
    19.4 KB · Views: 149
Hamna mkuu hujanielewa.. yaani nmemaanisha bikra itakua kama credit vile.. kwa mfano wakigombea 10 sasa yule ambae ni bikra ndie ntaemuoa.. na pesa haina mwenywe naamini ipo cku tu na mie ntaipata

Labda kama unaongelea bikra ya Kichina
 
Mheshimiwa Rais, nimefurahishwa vilivyo na jinsi ulivyoanza uongozi wako wa awamu ya nne kwa ziara za kushtukiza unazozifanya sehemu mbalimbali ambazo unahisi kuna matatizo yanayowaelemea wananchi. Kwa jambo hilo nakupa hongera sana. Wasiwasi wangu ni kwamba, je,baada ya ziara kama hizo ufumbuzi wa matatizo uliyoyaona utapatikana kwa wakati wake? Mfano; Muhimbili wagonjwa kulala chini, mpaka leo hatujasikia hatua zilizochukuliwa. Je, Vitanda vitapatikana lini?

Umeme bei juu lini utapunguzwa? Au ni kutokana na hii hali ya ukame…labda! Na kule kwenda sokoni na kuona bei ya vyakula kuwa juu, je kwa kauli yako wafanya biashara wamefanya lolote kupunguza bei? Mheshimiwa nafikiri wakati umefika wa kuwatumia wasaidizi wako wafanye kwanza utafiti wa kina wa matatizo ya sehemu unazoziona zina shida, ili unapotembelea sehemu hizo utoe hitimisho na kauli zilizofanyiwa utafiti wa kina. Kwa bahati mbaya Mheshimiwa rais nchi yetu ina matatizo mengi sana kila nyanja, nachelea kusema kwamba sehemu ambazo utakuwa hujatembelea wajanja watatumia kigezo hicho kwamba hawajaonekana hivyo kuzidi kutunyanyasa. Pia kama ziara hazitakuwa na ukali wa utekelezaji, basi wataona ni kawaida ya rais kututembelea na kuongea...!

Kuna jambo lingine tena Mtukufu Rais ambalo ni muhimu kwako kuliangalia, UWAJIBIKAJI WA PAMOJA (total responsibility). Serikali yako bado ni changa sana madarakakani hivyo inahitaji mawasilianao ya karibu sana katika utendaji wake ili kuimarisha msingi wa mtandao wa utekelezaji wa yale manayoyakusudia. Kitendo cha hivi karibuni cha wewe kwenda kutembelea daraja la muda bila kuwepo kwa mhusika yeyote wa ngazi za juu katika wizara inayohusika, ni cha kushangaza na kuacha maswali mengi nyuma.

Yako mengi sana Mheshimiwa yanayonipa mashaka na maswali mengi kichwani kama kauli zinazopingana kuhusu wafanyabiasha wadogo (wamachinga), Namna zoezi la ukamataji wa wafanyabiashara wanaohusishwa na ujambazi unavyofanyika na hatima yake….ni megi, mengi…nitarudi tena mhesimiwa rais.

ngatuni.

Kwa hiyo ndugu zako watakua wanalea M
mume na mke duuuu! Kazi wanayo.
 
Hamna mkuu hujanielewa.. yaani nmemaanisha bikra itakua kama credit vile.. kwa mfano wakigombea 10 sasa yule ambae ni bikra ndie ntaemuoa.. na pesa haina mwenywe naamini ipo cku tu na mie ntaipata

Hata ambaye hana bikra utampata.
Naomba tarehe tano ulete mlejesho.
 
Umepanga chumba Usagara na hicho chumba pia unalipiwa na ndugu? sasa mke akija kwako ajitegemee yeye na wewe mpaka utakapo shushiwa hiyo pesa eeh? na deadline juu na awe hivi awe vile hela huna,sasa mtoto pia Mke na ndugu zako watalea? yani wakulee wewe na mwanao na demand kibao.
 
umepanga chumba Usagara na hicho chumba pia unalipiwa na ndugu? sasa mke akija kwako ajitegemee yeye na wewe mpaka utakapo shushiwa hiyo pesa eeh? na deadline juu na awe hivi awe vile hela huna.
sasa mtoto pia Mke na ndugu zako watalea? yani wakulee wewe na mwanao na demand kibao........

‪Wifi umenikumbusha nyimbo Ya Baikoko, wenzangu zao wananunuliwa Corolla, Mie yangu inamaana Gani? Naitia moto... ����
 
‪wifi umenikumbusha nyimbo Ya Baikoko, wenzangu zao wananunuliwa Corolla, Mie yangu inamaana Gani? Naitia moto... 
Pande la wifi salam Aleykum,mwenzangu yani maisha huna unataka kuoa zile zile style za Udugu ni pesa...
 
Hamna mkuu hujanielewa.. yaani nmemaanisha bikra itakua kama credit vile.. kwa mfano wakigombea 10 sasa yule ambae ni bikra ndie ntaemuoa.. na pesa haina mwenywe naamini ipo cku tu na mie ntaipata

Haha eti wakigombea
 
Labda kama unaongelea bikra ya Kichina

Hata ya kichina hapati! nani atakubali kugharamika na bikra kwa zigo kama hilo?
Huyu jamaa ni anajifanya mjanja tu, nia yake apate sugarmamy alelewe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom