Mheshimiwa Rais, nimefurahishwa vilivyo na jinsi ulivyoanza uongozi wako wa awamu ya nne kwa ziara za kushtukiza unazozifanya sehemu mbalimbali ambazo unahisi kuna matatizo yanayowaelemea wananchi. Kwa jambo hilo nakupa hongera sana. Wasiwasi wangu ni kwamba, je,baada ya ziara kama hizo ufumbuzi wa matatizo uliyoyaona utapatikana kwa wakati wake? Mfano; Muhimbili wagonjwa kulala chini, mpaka leo hatujasikia hatua zilizochukuliwa. Je, Vitanda vitapatikana lini?
Umeme bei juu lini utapunguzwa? Au ni kutokana na hii hali ya ukame…labda! Na kule kwenda sokoni na kuona bei ya vyakula kuwa juu, je kwa kauli yako wafanya biashara wamefanya lolote kupunguza bei? Mheshimiwa nafikiri wakati umefika wa kuwatumia wasaidizi wako wafanye kwanza utafiti wa kina wa matatizo ya sehemu unazoziona zina shida, ili unapotembelea sehemu hizo utoe hitimisho na kauli zilizofanyiwa utafiti wa kina. Kwa bahati mbaya Mheshimiwa rais nchi yetu ina matatizo mengi sana kila nyanja, nachelea kusema kwamba sehemu ambazo utakuwa hujatembelea wajanja watatumia kigezo hicho kwamba hawajaonekana hivyo kuzidi kutunyanyasa. Pia kama ziara hazitakuwa na ukali wa utekelezaji, basi wataona ni kawaida ya rais kututembelea na kuongea...!
Kuna jambo lingine tena Mtukufu Rais ambalo ni muhimu kwako kuliangalia, UWAJIBIKAJI WA PAMOJA (total responsibility). Serikali yako bado ni changa sana madarakakani hivyo inahitaji mawasilianao ya karibu sana katika utendaji wake ili kuimarisha msingi wa mtandao wa utekelezaji wa yale manayoyakusudia. Kitendo cha hivi karibuni cha wewe kwenda kutembelea daraja la muda bila kuwepo kwa mhusika yeyote wa ngazi za juu katika wizara inayohusika, ni cha kushangaza na kuacha maswali mengi nyuma.
Yako mengi sana Mheshimiwa yanayonipa mashaka na maswali mengi kichwani kama kauli zinazopingana kuhusu wafanyabiasha wadogo (wamachinga), Namna zoezi la ukamataji wa wafanyabiashara wanaohusishwa na ujambazi unavyofanyika na hatima yake….ni megi, mengi…nitarudi tena mhesimiwa rais.
ngatuni.