Natafuta Mke aliyeathirika na virusi vya UKIMWI

Status
Not open for further replies.
Mungu akupe hitaji la moyo wako. Wale mnaobeza hujafa hujaumbika. Kuna wewe, wazazi, ndugu, marafiki na Watoto. Utaguswa tu na HIV/AIDS.
 
Hapo sasa ndio usemi unakamilika wa
“UKIMWAGA MBOGA NAMWAGA UGALI”

Hakuna hata mmoja aliejitokeza,,,kweli imani unazipima kwa kitu kidogo mno
 
Aisee bro, ningekushauri kitu kimoja. Nenda kwenye vituo vya ushauri au hizi CTC Center onana na wale wahusika unawaeleza kuwa mimi nina hali hii ila ninahitaji kupata mwenzangu wa ndoa. Wale huwa wanakutanisha watu wenye uhitaji wa namna hiyo. Kuna ndugu yangu alikuwa anapata huduma ya ARV's kwenye kituo kimoja hivi, alimweleza yule nurse pale kituoni hata haikuchukua muda alimkutanisha na dada mmoja na tayari wameshafunga ndoa. Siku aliyoenda alikuta kuna wadada kadhaa walikuwa wameacha picha zao na contacts kwa yule mhudumu..... Mungu akutangulie!
Mkuu nadhani nifuate ushauri wako
 
Wakuu Kichwa kinajieleza. Nina Miaka 36
1. Awe Mkristo (Sio Msabato)
2. Umri miaka 25-30
3. Ikiwa ana Mtoto asizidi mmoja
4. Awe mnene asiwe mwembamba
5. Kabila lolote.
NITAKAPOKUWA NIMEMPATA NITAOMBA MODERATORS WAUFUNGE HUU UZI KWAHIYO MKIONA HAUJAFUNGWA MAANA YAKE BADO HAJAPATIKANA
Mwenye hizo sifa ani PM
Sawa mkuu ngoja tusubili waje
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom