Allency
JF-Expert Member
- Jan 27, 2011
- 13,729
- 13,097
Sawa mkuu umesikika, haya wewe una maarifa gani?Typing error. Neno la kiswahili ni Shahada.
Niwashauri vijana wa miaka ya hivi karibuni kwamba,, unaposoma andiko fulani, jikite zaidi kuuelewa ujumbe uliopo kwenye andiko hilo na sio usome huku ukitafuta cha kukosoa kwenye andiko hilo, tabia hii ni ujinga wa hali ya juu sana. Mwenye kutaka maarifa atanielewa namaanisha nini na atajitafakali lakini mpumbavu ataendelea kukosoa makosa ya kimaandishi badala ya kukosoa ujumbe uliomo kwenye andiko kisha kutoa maoni yake.
Nitolee mfano,
Mtu mmoja hapo juu kauliza, " mwezi April ulikuwa na diploma, leo September una bachelor?, Tuambie hicho chuo kinachotoa bachelor ndani ya miezi minne."
Ni hivi , kipindi naandika ujumbe huo nilikuwa ninamiliki cheti cha diploma wakati huohuo nikiwa mwaka wa tatu nikimalizia kusoma Bachelor Degree in........, Na sasa nimemaliza na matokeo yametoka sina supplimentary, unadhani leo nilipoandika andiko hilo ningesema kwa sasa nina diploma ???.
Kwa mtu mwenye akili na mwenye kufikilia kabla ya kutenda angejiuliza maswali kadhaa kabla ya kukutupuka kuja kuhoji swali la kitoto kama hilo.
Binafsi mtu huyo na mwingine wa aina hiyo nimewaza na kuwaona ni wapumbavu, walikwenda shule kujifunza ujinga, walikwenda shule kuchukua cheti na si maarifa, ndio hao wanaoshinda vijiweni wakiilalamikia serikali haiwapi ajira wakati serikali iliwapa mikopo wakasoma akili zao zinawatuma serikali iliowapa mikopo ndo hiyo hiyo wanasubiri iwape na ajira pia na ndio hao hao wanaotaka kazi za raha raha tu hususani za kukaa ofisini wakiwaza kuiibia serikali na kupiga madili, wanaamini msomi yeyote alitoka kimaisha kwa njia za madili tu na sii taaluma na uwezo wake, ni watu pia wanaoamini kazi hupatikana kwa njia ya CONNECTION na si uwezo binafsi, ndio maana wamegeuka kuwa na wasomi "makasuku" wanaokariri bila kufikiri, Fikra zao ni Tasa, hazigawanyiki kuwaza mambo kwa upana zaidi.
Niwatakie jioni njema wale wenye akili na maarifa lakini kwa wale wajinga wanaojiona kuwa wao ni sahihi kwa kila kitu waendelee kubanua madomo yao vijiweni.