Natafuta mchumba

Natafuta mchumba

ilisha juniour

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
714
Reaction score
219
Natafuta mchumba ambaye hana uzazi na ambaye atakuwa tayari tufunge ndoa baada ya kufahamiana,nipo Kanda ya Ziwa kikazi,Umri miaka 30,elimu yangu ni chuo kipato cha wastani.

Napenda awe na umri kuanzia miaka 26 asizidi 35,awe amejiajiri ama kuajiriwa elimu kidato cha nne na kuendelea,

Mambo mengine tutawasiliana zaidi kwa pm.

Naomba kuwasilisha
.
 
wana haki pia ya kupendwa kaka,na kwakuwa nao ni binadamu nna imani ntampata
 
natafuta mchumba ambaye ni tasa na ambaye atakuwa tyari tufunge ndoa baada ya kufahamiana,nipo kanda ya ziwa kikazi,umri miaka 30,elimu yangu ni chuo kipato cha wastani,napenda awe na umri kuanzia miaka 26 asizidi 35,awe amejiajiri ama kuajiriwa elimu kidato cha nne na kuendelea,mambo mengine tutawasiliana zaidi kwa pm,naomba kuwasilisha

Si dhan kama kuna atayejitokeza.
Wewe ni mfuasi mzuri wa dini?
Me nadhan ungenuliza ki vingine.
 
tasa? why? Isije ikawa na matasa wameanza kuwa dili kama albinos
 
Mambo ya kanda ya ziwa yanatisha usikute masharti ya mganga hayo au unataka kumtoa sadaka bint wa watu,kuweni makin mabinti
 
kwa maana ipi?,

Hako ka ombi kako kama ki unyanyapaa flan hizi.
Ni kweli uwazi ni mzuri ila usingesema "Tasa" labda ungesema ambaye hapati mtoto
Nooo hiyo nayo haiko poa yn sijui ingetumika lugha gani
Ila hiyo uliyotumia ngumu sana.
 
Hako ka ombi kako kama ki unyanyapaa flan hizi.
Ni kweli uwazi ni mzuri ila usingesema "Tasa" labda ungesema ambaye hapati mtoto
Nooo hiyo nayo haiko poa yn sijui ingetumika lugha gani
Ila hiyo uliyotumia ngumu sana.

ok nimekuelewa ila nimefikiria sana nikaona tu niiweke wazi maana unaweza tumia neno lolote ila maana inabaki pale pale nadhani tupo pamoja
 
wana haki pia ya kupendwa kaka,na kwakuwa nao ni binadamu nna imani ntampata
Sijaelewa sehemu moja! Yaani kutokuwa na uzazi ni condition au wewe una matatizo ya uzazi kwahiyo unahitaji asiye na uzazi mwenzako ili pasiwe na unyanyapaa kati yenu?! Au may be una matatizo ambayo yanaweza kuhatarisha uhai wako endapo unashika ujauzito (am assuming ni mwanamke manake huja-specify)!

Kama ndio, mie sidhani kama ni sahihi kutoa hiyo condition coz' wapo wenye uzazi ambao hawaoni taabu kuoa asiye na kizazi... wengine real love kwanza hayo mengine ni matokeo tu! Mathalani kwa upande wangu, na wala sio kwamba najipigia chapuo, sidhani kama naweza kuja kuacha au kumnyanyapaa mwanamke simply because hana uwezo wa kushika mimba!
 
Enendeni ulimwenguni mkazae mjaze dunia haya siyo maneno yangu ni maandiko matakatifu sasa wewe hutaki azae kwa nini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom