Natafuta mbia wa kuanzisha nae biashara ya App

Joined
Apr 12, 2017
Posts
9
Reaction score
3
Salam JF,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza.Mimi ni mbunifu wa Applications mbalimbali za simu na smart devices nyingine kwa ajili ya kuboresha na kurahisisha maisha ya watu na pia ili kwenda sambamba na teknolojia.

Sekta ya teknolojia ya mawaailiano katika maisha ya watanzania inakua kila uchao. Hivyo, kama kijana nimeiona fursa hiyo na kujikita kwenye tafiti za applications mbalimbali ambazo zinaweza kurahisisha maisha ya watu na pia kujitajirisha.

Katika tafiti zangu nimekuja na wazo ambalo lipo katika hatua ya utekelezaji kwa kuwa limeshasanifiwa na programmers.

Kama ilivyo kwa biashara nyingine hata biashara ya Apps inahitaji mtaji ili kuanza kuzalisha pesa. Katika kutekeleza mradi huo nimepungukiwa pesa ili kukamilisha mradi huo.

Hivyo basi, nimeona nitumie jukwaa hili ili kutafuta mtu makini atakayekuwa tayari kuwekeza katika mradi huu.

Ili kujua app hiyo inafanya nini na itatengenezaje pesa inatakiwa tukutane ana kwa ana kwa ajili ya mazungumzo.Kabla ya kukufafanulia kwa undani juu ya app hiyo nitakupatia NON DISCLOSURE AGREEMENT (mkataba utakaokufunga usitoe siri za biashara hiyo ). Ukisaini mkataba huo ndipo tutazungumzia app hiyo kwa undani na usiposaini itakuwa ndio mwisho wa mazungumzo yetu.

Kabla ya kuusaini mkataba huo utakuwa huru kuupeleka kwa mwanasheria yoyote unaemuamini ausome kisha akushauri kama usaini au usisaini. Lengo la mkataba huo ni kukuzuia usitoe siri za biashara hii kama hatutaafikiana kufanya kazi pamoja au usipokubaliana na wazo la biashara.

Endapo utasaini mkataba huo tutaizungumzia biashara hii kwa kina na usipoipenda au usipokubaliana nayo hautalazimishwa kufanya biashara hiyo ,lakini utakuwa na wajibu wa kutunza siri za biashara hii vinginevyo sheria itachukua mkondo wake.

Endapo utasaini mkataba huo na tukaizungumzia biashara hii kwa kina na ukakubaliana nayo itabidi twende hatua ya pili ambayo ni kuanzisha kampuni ya pamoja (Joint Venture Company) ambayo wewe utamiliki 30% ya hisa zote za kampuni.

Kampuni hii ndio itakayoendesha biashara tajwa kwa ushirikiano wa pamoja. Pesa utakazotoa zitatumika kumalizia posho za vijana wanaofanya creation ya app, taratibu zote za TCRA n.k

Pesa unayotakiwa kuchangia ni Tsh. 10,000,0000/-. Sio lazima ukawa mtu mmoja ,pesa hiyo inaweza kutolewa au kuchangwa na mtu zaidi ya mmoja na mkagawana 30% ya hisa za kampuni kadri ya michango yenu.

Kutokana utafiti niliofanya app hii inakadiliwa kuweza kuzalisha kati ya Tsh. 10,000,000/- hadi 15,000,000/- kwa mwezi katika hatua za miezi sita ya kwanza na kukua hadi 50,000,000/- kwa mwezi baada ya kufanya kazi zaidi ya miezi 12 ya kwanza. (Haya ni maoteo tu).

NB. Bandiko hili ni salama na halina udanganyifu wowote ndio maana mchakato wake unahusisha wanasheria na pia huruhusiwi kutoa hela yoyote kama hautakubaliana na biashara. Na ukikubaliana na biashara pesa hizo zitawekwa kwenye akaunti ya pamoja au pesa zote utabaki nazo na utakuwa unafanya malipo ya kila kazi pale pesa zinapohitajika tu.
 
Just idea au pia una Hard Cash??? Im interested but need to know more before I put my feets
 
Mkuu nitumie namba yako PM naweza kukupeleka kwa mtu flani yeye mdau mkubwa wa hizi mambo anaweza kuwekeza akiridhika na proposal zako.
 
Yani ni saini kitu nisichokijua!
Soma vizuri uzi huu kabla ya kucoment mkuu. Nimesema kabla hujasaini peleka mkataba kwa mwamasheria wako akufafanulie, majibu yake yatakufanya ujue kama utasaini au laa.haulazimishwi kisaini.
 
Nadhani Hujamuelewa Mkuu @sijutii
Kwenye post yako unasema baada ya mtu kusaini mkataba ndiyo unamwambia hiyo idea.!!!(Tatizo Hilo)..

Na pia wewe mtoa idea inapaswa umiliki 50% na mtoa pesa inapaswa amiliki 50%..
 
Mkuu mkataba unaosainiwa kabla ya kujua undani wa biashara ni mkataba unaomfunga mpokea hoja kutunza siri ya biashara yenyewe na si mkataba wa ubia.

Kuhusu kiwango cha hisa ni kama nilivyoeleza hapo juu 30% hii ni kutokana na sababu ambazo siwezi kiziweka hapa.
 
Safi sana mkuu, unaonekana uko serious kwa kuweka utaratibu wa kisheria. Hope utapata partner soon .kila la heri.
 
Back
Top Bottom