Natafuta mbia (hata zaidi ya mmoja) wa biashara ya nafaka na mafuta

me1

JF-Expert Member
Jan 24, 2015
367
421
Habari wanajamvi,

Kwenye mahangaiko yangu nina viduka kadhaa sehemu mbalimbali mkoani DSM.Ndoto yangu ni kuwa na matawi Dar nzima.

Nime-specialize kwenye uuzaji wa Unga wa SEMBE/DONA, CHAKULA CHA MIFUGO na MIKATE na VITAFUNWA (Bakery).

Lengo la kuleta uzi huu ni kuwa sitaki kabisa kuchanganya mambo na hivyo sihitaji kuchanganya biashara zingine na hivyo nakaribisha wawekezaji walioko serious tufanye kazi.

Maduka yangu yanakuwa na sifa hizi.

1. Yanakuwa maeneo changamfu mfano: Chanika mwisho njia panda ya Mbagala na Masaki.

2. Maduka yamelipiwa kodi, yana leseni ya hiashara na TIN

3. Maduka ya EFD kwa ajili ya compliance ya mambo ya jamhuri

4. Maduka yana muuzaji tayari.


Sasa nahitaji mbia wa kufanya nae biashara kwa condition zifuatazo:

1. Biashara yake lazima iwe ya Chakula ( Mfano:Mafuta ya kula, Mchele, Maharage, Ulezi, Lishe, Mayai n.k)

2. Biashara lazima iwe na bei ya chini kidogo kuliko bei za sokoni ili kuongeza kasi ya mzunguko na awe tayari kuwauzia wanunuzi wa jumla kwa bei za jumla)

3. Kwa bidhaa ambazo ni rahisi kuzi- brand basi itakuwa ni vyema zikiwa branded. Mfano LISHE, MCHELE, Unga wa Muhogo n.k

4. Lazima akubali kushare cost zitakazo poza maumivu kwenye uwekezaji uliofanyika (Hii ni makubaliano)

NAMNA YA UENDESHAJI

- Mbia ataingia ubia na sisi na kupata report ya mauzo kila siku na kupata pesa yake kwa njia atakayochagua kila siku.

- Risk ya mzigo na pesa itakuwa kwetu kwa kipindi chote cha biashara

- Mbia anaruhusiwa kufanya promotions za aina yoyote na kuliita dula la kwake pasi na kizuizi

- Mbia atachagua maduka anayotaka kuweka biashara yake

- Ubia huu hauna mgawanyo wa faida na hivyo bills zote zitakuwa fixed pasi kujali mwenendo wa boashara.

- Mbia hawezi kuleta biadhaa iliyoletwa na mwingine. Mfano kama dukani kuna mafuta, huwezi tena kuleta mafuta.


Conditions zingine ni Makubaliano yanayozungumzika.


Niko PM nawasubiri kwa mazungumzo zaidi na mawasiliano.

Karibuni sana tuijenge Nchi.
 
Hapa umeandika utopolo tuu... mimi ni mfanyabiashara wa nafaka lakini kwa hapa hakuna mjinga utakayempata
 
Supplier akubali kukuuzia kwa bei ya chini kidogo na akubali wewe kuuzia wateja wako/wenu kwa bei ya jumla. Yani pamoja na kukuuzia jumla kwa bei ya chini kidogo, bado aruhusu mteja mwingine auziwe bei ya jumla. That means hiyo bei iwe ya jumla kweli.

Kisha mnafanya kugawana cost ili kupoza maumivu ya uwekezaji wako.

Bills ziko fixed bila kujali mwenendo wa biashara.

Sitaki kusema kitu. Suppliers njooni
 
Back
Top Bottom