Natafuta mbegu nzuri za Migomba kwa Dar es Salaam

Karibu tukuhudumie mkuu, niko SUA Horticulture. Tuna miche ya matunda lakini pia migomba ipo, bei ya mche ni sh 3500 lakini ukichukua kuanzia miche 50 bei ni sh 2500.

Gharama za usafiri kutoka Moro-Dar kwa pacel moja ni sh 13000. Ambapo pacel moja inakuwa na miche isiyozidi 50.

Mchanganuo wa nauli
3000- ni nauli ya boda kutoka SUA mpaka Msamvu
1000- Kitorori ndani ya stend
11000- nauli Moro-Dar

Namba zangu 0719527062/0757056472 karibu Pm pia kwa maswali na maelezo zaidi
Shukuran sana nitawasiliana na wewe mkuu baada ya mwaka mpya TUKIJALIWA
 
Kuhusu magonjwa ya migomba yapo mawili Kuna Panama wilt au Xanthomonas wilt uliathiri maeneo ya Bukoba wakapigwa Quarantine ya kusafirisha kwenye mipaka ya mkoa then pale kituo cha utafiti wa ndizi wakaanza kuzalisha aina ya fhia au Fia na hapa zipo nyingi 1,2,3,17,19 na 21 na matoleo mengine meengi shida watu wanalalamika ladha sio nzuri hasa wa maeneo husika. Hizi series kwa kanda ya mashariki utapata moja tu ambayo ni Fhia 19.

Kuna wilt ya bacteria kama sijakosea kwa haraka ila hii inaathiri ndizi fupi au kiujumla zinaitwa Cavendish kama vile Malindi,mtwike,William na Grandnain.
Sasa hapa kilichopo ni Vice versa kuwa aina zinazoathiriwa na Bacterial diseases zinakuwa zinakinzana na Panama na zinazonkinzana na Panama zinaathiriwa na Bacterial.

Shida kubwa inatokea ni muda wa kuhudumia shamba kupitia vifaa kama vile kisu au jembe ndio husambaza magonjwa yote ya aina mbili na huku mtaani inatembea ikiwa maandalizi ya kuandaa miche yaani vile vifaa visipowekewa kinga na hapa kuna namna yake ya kuandaa miche.
Kudhibiti magonjwa ukiacha suala la usafi katika shamba na Mali shamba bhas pia kuna njia ya kimaabara ya kuzalisha niche isiyo na maambukizi nayo ni tissue culture au migomba ya maabara.
Niishie hapa kwa Leo.
 
Piga 0714600575/0620598113 kwa ushauri Wa kina na migomba. Karibu


Moja ya matatizo ya migomba ni kuchukua katika chanzo kisichojulikana mwisho ikianza kusumbua hauna wa kumlaumu.
Mavuno bora yanaanzia na mbegu safi
Wajumbe natumaini hamjambo.

Naomba kwa yeyote anayejua namna ya kupata mbegu nzuri ya migomba kwa maeneo ya karibu ndani ya jiji hili la DAR

Mahitaji yangu sio makubwa kama 100 hadi 200 kwa kuanzia. Ziwe za kupika na kuivisha pia.
 
Magonjwa yapo matatu kwa Dar ni black cigatoka ndio inatafuna.

Athari yake ni kuathiri ukubwa wa mikungu ya migomba
Pia sasa hivi kuna ugonjwa umeingia kwenye migomba sijajua ni ugonjwa gani, upo sana maeneo ya Dar huko sijui unafahamu hilo mkuu?
 
Tunagawanya migomba kutokana na uwezo wa kukinzana na magonjwa na matumizi yake kama za kupikwa,mbivu na kuchoma
Shukrani sana mkuu bahati mbaya aina zilizo nzuri sizijui kwa majina labda kama kuna yeyote humu anayejua majina anisaidie baadhi ni kama SHAKALA , WILLIAM, FHIA 17, MZUZU
 
Back
Top Bottom