Natafuta mbegu bora ya mbaazi

kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
502
938
Wanabodi, salaam! Wapi nitapata mbegu bora ya kisasa ya mbaazi? Nimepita maduka mbalimbali ya mbegu, nimekosa. Nimeenda hadi TARI-Ilonga, Kilosa (Taasisi ya serikali ya kuzalisha mbegu) nimekosa pia. Mbegu ninayoihitaji ni ile mbegu ya muda mfupi

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
 
Asa umeenda?
Ukikosa na kwa hao jamaa. Inabidi uende kwa wakulima sasa. Manyara na Kibaigwa huwezi kosa hiyo mbegu. Hakikisha ni mbaazi nyeupe ndo yenye bei nzuri sokoni
Hizo mbaazi nyeupe kwa Dar naweza kupata wapi? Nataka kulima chache za kula na kugawa kwa ndugu wa karibu
 
Mbegu bora zinapatikana kwenye maduka ya pembejeo. Humu kuna watu wana uzoefu ndio maana nimeuliza ili nipate wanapouza specifically
Samahani kama jibu limekukwaza la kukuambia uende sokoni. Ila kama umefuatilia huu mjadala utaona sehemu zote wanazo andaa na kuuza hiyo mbegu hawana. Na kwa kua wewe unahitaji kupanda za kula tu na si kibiashara. Hata zinazo uzwa sokoni zinafaa vizuri tu
 
Hujanikwaza ndugu yangu na hata hivyo jibu lako limenisaidia sana maana nitanunua za sokoni kwa kesho na kuzipanda wiki hii shambani. Naendelea kutafuta mbegu bora ila hizo za sokoni nitazifuatilia ukuaji wake pia zikiota vizuri naendelea nazo
 
Wanabodi, salaam! Wapi nitapata mbegu bora ya kisasa ya mbaazi? Nimepita maduka mbalimbali ya mbegu, nimekosa. Nimeenda hadi TARI-Ilonga, Kilosa (Taasisi ya serikali ya kuzalisha mbegu) nimekosa pia. Mbegu ninayoihitaji ni ile mbegu ya muda mfupi

Sent from my Infinix X6816 using JamiiForums mobile app
Kama unaweza kufika mpaka Kilosa huwezi kushindwa kufika Morogoro. Nenda ASA pale Morogoro ndicho kiwanda cha
kufungasha mbegu kwa Tanzania. Wana mbegu za kila aina!
 
Nimetoka ASA leo hii, hiyo mbegu hawana pale. Wamejaza mbegu za mpunga na alizeti za kutosha
 
Back
Top Bottom