Njia ngumu lakini yenye tija, nimeifanya kwa kuku wa kawaida, nafikiria kuifanya kwa chotara kwenye mwezi wa kwanza Mungu akitupa uhai.
Tafuta tetea wazazi kama watano wanaotaga, na jogoo la kienyeji toka koo nzuri, utapata kizazi cha kwanza tukiite F1. Chagua majike bora toka F1, yaweke na jogoo la kuku mzazi. Utapata F2. Ukirudia utapata F3 ...F4. Mpaka F4 utakua na kizazi bora cha kuku chotara kuliko wengi waliopo mitaani, utagaji utakua juu, uwezo wa kutengeneza nyama mkubwa, ila watakua na uwezo mdogo wa kuatamia na kutunza watoto.
N.b. Kuku wazazi wa nyama ni kizazi kimoja kabla ya kuku wa nyama.
Unaweza kutumia njia hii kwa mshazari na njia unayoonekana umeichagua tayari.
Salaam.