Natafuta kazi yoyote ya halali nina elimu ya Astashahada ya Electrical and Automation

Kijana Jr

JF-Expert Member
May 12, 2016
560
838
Habari za humu ndani wote ni wazima,

Kwa mara nyingine tena kijana wenu nakuja kwenye jukwaa hili kuomba nafasi yoyote ya kazi ambayo itakuwa halali.

Mimi ni mwanaume mwenye umri wa miaka 27, Elimu yangu nina certificate of electrical and automation. Nimekuja hapa kwa mara nyingine kuomba kwa yoyote aliye na kazi au aliyesikia kazi mahali popote pale sichagui kazi yoyote nitafanya iwe ya halali tu.

Ninaweza kufanya kazi za ufundi umeme majumbani na maofisini au Msaidizi wa fundi umeme. Nina kipaji cha kufundisha core subject na patiko ya electrical katika Vocation school kwa level one na level two au kwa yeyoto mwenye hitaji la kujua umeme (wewe au mwanao)

Napatikana Dar es Salaam ilala kwa aliye tayari aniambie ili tupeane mawasiliano. Niko serious ndugu zangu, hata mtu akiniambia niende kesho nikafanye kazi naenda tu.

Mungu awabariki sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kijana nakushauri, usiombe kazi kijumla jumla "kazi yoyote", kuwa "specific", kwani hakuna duniani awezae kazi zote.

Andika hivi, naomba kazi zozote kati ya hizi au zinazofanana nazo, upishi, msaidizi wa mpishi, mfanya usafi wa ndani na nje, mtunza bustani, kazi za ufundi umeme majumbani na maofisini au Msaidizi wa fundi umeme...

Unaweza ziainisha kazi ambazo ukipewa utazifanya kwa ufanisi.


Ni ushauri tu.
 
Back
Top Bottom