Natafuta kazi ya Udereva

MoonBoy

Senior Member
Jul 15, 2016
188
250
Naitwa Rashidi omary Khatibu, umri wangu miaka 27, Mzawa wa tanga... Ila kwa sasa naishi Arusha

Kazi niliokua nafanya ni kusafirisha mizigo mbalimbali kwenda mikoani kwa njia ya maroli, nikiwa kama dereva... Ila kwenye kazi kama mnavyojua hazikosi kasumba ndogondogo.

Nina mwezi wa sita sasa toka nimesimamishwa kazi.. Nimezunguka Arusha nzima hii... Kazi ni ngumu. Mpaka siku ya jana, nimejikuta tu nimeingia mpaka kwenye nyumba binafsi nikajua ni kampuni,... Yote hio ni shida na ukosefu wa kazi.

Ndugu zangu, Kiukweli mimi ni mwanaume kama nyinyi... Naombeni mwenye ramani ya kazi ya udereva wa gari yeyote kasoro SEMI tu.. Mana sikuwahi kulitumikia... Gari yeyote jamani Naendesha... Leseni yangu imejaa madaraja yote kasoro pikipiki tu... Na cheti cha veta ninacho cha CLASS C

Nipo jijini Arusha.... Naombeni msinikebei ndugu zangu... Mana nimemaliza mji.. Naona niombe ndugu zangu humu ndani...

Tafadhali kama una ramani... Nicheki INBOX.. Tusaidiane wanaume wenzangu... Asanteni

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 

Pyepyepye

JF-Expert Member
Jan 6, 2017
1,941
2,000
Mungu akutendee.
Najua hali unayoipitia, nimepita katika mapito hayo pia.
 

Pyepyepye

JF-Expert Member
Jan 6, 2017
1,941
2,000
Shukrani ndugu yangu,... Napitia changamoto ngumu mpaka nahisi niko peke angu mwenye shida

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
Nimewahi kudondosha chozi kwa sababu ya ugumu wa maisha.
Nimesoma ujumbe wako, nimeelwa mapito yako. Sina chochote cha kukupa, ila itoshe tu kusema MUNGU akutendee kwa kadri ya imani na hitaji lako.
Najua hapa ni nyumbani kwa kila mtu.
Wako watu watatusaidia kutatua tatizo hili mkuu
 

MoonBoy

Senior Member
Jul 15, 2016
188
250
Nimewahi kudondosha chozi kwa sababu ya ugumu wa maisha.
Nimesoma ujumbe wako, nimeelwa mapito yako. Sina chochote cha kukupa, ila itoshe tu kusema MUNGU akutendee kwa kadri ya imani na hitaji lako.
Najua hapa ni nyumbani kwa kila mtu.
Wako watu watatusaidia kutatua tatizo hili mkuu
Asante sana ndugu

Sent from my Infinix Zero 3 using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom