Natafuta kazi ya muda

Mwalimu Truth

Member
Feb 15, 2015
57
62
Hello, Habari,

Natafuta kazi ambayo ninaweza kuifanya kwa malipo yeyote kadri ambavyo tutakubaliana na muajiri kulingana na ratiba yangu.

Umri: Miaka 27
Elimu Diploma ya Ualimu wa Sekondari somo la Baiolojia.

Jinsia: Me.

Uzoefu: Miaka 3 Mwalimu wa shirika la Compassion kazi ambayo bado ninaifanya mpaka sasa.

✓Uzoefu wa mwaka mmoja kufundisha shule za English Medium

Muda wa Kufanya kazi: Niko free jumatatu mpaka jumatano kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa tisa kamili, kuanzia saa kumi na moja kamili jioni mpaka usiku.

Alhamisi na ijumaa niko free sina kazi.

Jumamosi, nakuwa kazini kwahiyo sina muda.

HIVYO BASI, mwajiri wangu kwa sasa ninamfanyia kazi jumatatu mpaka jumatano kwa masaa mawili kila siku, saa tisa mpaka saa kumi na moja kamili pamoja na siku yote ya jumamosi.

Kazi ninayoitafuta ni kwa masaa ambayo ninakuwa free ili kuongeza kipato cha ziada.Natafuta kazi kwenye Sheli za mafuta, Lodge,Hotels,Shule binafsi, Maduka binafsi na taasisi zozote ambazo zinaweza kunipatia kazi kulingana na ratiba yangu hiyo. Naweza kufanya kazi muda wa usiku pia.

Mahali: Niko Kasulu,Kigoma.

NATANGULIZA SHUKRANI.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom