Mkuu pole sana.kuna wakati huwa nawaambia vijana kuwa shule na mtaani ni dunia mbili tofauti japo zinafanana,kuathiriana na kukamilishana.
Ushauri wangu kwa sasa ukiwa bado unatafta uajiriwe hebu fanya yafuatayo
1.Kusanya wenzako watano wasio na kazi waliosoma kozi kama yako au IT.
2.Tafteni sh.30,000 kila mmoja(najua huna pesa ila unaweza kuomba kwa ndugu rafiki au jirani au kuangalia any redundant asset ulio nayo ambayo huna matumizi nayo na iuze upate mtaji).jumla mtakuwa na sh.150,000
4.Tafteni fremu uswahilini isiyozidi 50,000 kwa mwezi
3.Fungueni ofisi ya kutengeneza vifaa vya electronics kama simu,computer nk. Toeni huduma za kuinstall software za simu na computer, burn cd, uzeni vifurushi vya tigo,voda nk
4.Kila mmoja aombe kiti kimoja nyumbani na alete ofisini
5.In case kama mmoja wenu alibahatika kununua friji akiwa chuo au analo nyumbani,basi lileteni ofisini na uzeni maji ya kufunga ya viroba. Kila kiroba ni sh 100. Pesa mtakayoipata kwa kuuza maji itawasaidia kupata nauli.
Baada ya miezi mitatu njoo hapa itupe mrejesho.
Kila la kheri
big up..kila post/reply kumi; Moja ingekuwa ya maana na nzito kama hii; jf ingekuwa moto wa kuotea mbali. hongera naamini kuna baadhi umewafungulia njia.