Natafuta kazi kwa mara nyingine tena

solanum

JF-Expert Member
Jul 28, 2015
203
99
Habarini wakuu!

Mimi ni mhitimu wa chuo kikuu nina bachelor degree of science in food science and technology nimemaliza mwaka jana (2015) nimeomba kazi sehemu mbalimbali lakini nimepata kuitwa interview sehemu moja tu nayo sikufanikiwa kupata kazi, mpaka sasa niko njia panda maisha yamezidi kuwa magumu kwangu hadi najuta kwanini nilisoma hii kozi.

Sasa jamani kama kuna yoyote mwenye kazi naomba anisaidie nipo Dar es salaam namba zangu 0758 106 501.
 
hy course yako kaz utapata si unaona ata interview unaitwa....kuna course mwaka mzima miaka miwil no interview...kazana kutafuta opportunities..kila la heri
 
Wewe ndo kwanza umemaliza mwaka jana na umefanikiwa japo kuitwa kwenye interview shukuru Mungu una bahati nzuri na kazi utapata soon.Wengine wana miaka wanatuma maombi bahasha zao zinawekwa pembeni tu hawajawahi kuitwa interview.
 
Hapa nilipo hata hela ya kula sina kujtolea nitaweza kweli

Sasa mkuu kama kazi hauna na bado pesa ya kula haipo na haupati uzoefu wowote. Si afadhali ujitolee upate uzoefu hata kama hauna hela lakini unapata uzoefu? Huwezi jua kwenye kujitolea chochote chaweza kutokea. Usikate tamaa.

Mie nilianza kwa kujitolea lakani hakuna hata mwezi mmoja ambao sikulipwa pesa, nikapata uzoefu baada ya mwaka nikapata kazi nyingine.
 
Mkuu papatua sn kwenye haya maviwanda ya usindikaji bila kuchoka...hata ukianza kwa kujitolea sio mbaya.
 
Sasa mkuu kama kazi hauna na bado pesa ya kula haipo na haupati uzoefu wowote. Si afadhali ujitolee upate uzoefu hata kama hauna hela lakini unapata uzoefu? Huwezi jua kwenye kujitolea chochote chaweza kutokea. Usikate tamaa.

Mie nilianza kwa kujitolea lakani hakuna hata mwezi mmoja ambao sikulipwa pesa, nikapata uzoefu baada ya mwaka nikapata kazi nyingine.
ahsante kwa ushauri mkuu
 
Janga la weng mkuu usikate tamaa bora hata ukakope kwenye microbank ufanye biashara au kilimo sio lazma ufanye kaz ulio somea
 
Back
Top Bottom