Natafuta House Manager

Natafuta House Manager

baharia 1

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2019
Posts
1,778
Reaction score
2,052
Natafuta mfanyakazi wa ndani

Habari za muda huu ndugu zangu, jamaa na marafiki.

Kutokana na mazingira ya kazi kuwa mengi, nimeamua kutafuta msaidizi wa kazi za ndani (House Manager) ambaye atasaidiana nami majukumu ya hapa nyumbani.

Lakini sifa za mfanyakazi huyu nimeziweka kidogo ki-special maana sitaki mambo ya kuleteana ganzi hapa mjini.

Vigezo na Sifa za Mwombaji:
Muonekano: Awe mweupe (rangi ya mtume), maana nataka nyumba iwe na mwanga muda wote hata umeme ukikatika.

Umri: Usizidi miaka 25. Nataka mtu mwenye nguvu za kupambana na vumbi, siyo wa kuugua mgongo kila saa tano.

Hali ya Familia: Awe hana mtoto na awe (Single). Sitaki majukumu ya ziada ya kuanza kutunza wajukuu wa watu hapa ndani.

Elimu: Awe amemaliza angalau Darasa la Saba. Kikubwa ajue kusoma na kuandika (ajue kutofautisha chumvi na sukari, na aweze kuandika orodha ya mahitaji bila kukosea).

Dini na Kabila: Mengine yote ni ziada, awe anatoka popote na anasali popote, mradi awe na hofu ya Mungu na awe na nidhamu ya hali ya juu.

Sifa ya Ziada: Awe anajua kupika chakula kikaiva (siyo kutupia tu), mcheshi, na mwenye uwezo wa kufuata maelekezo bila kubisha.

Zingatia: Sifa hizi ni kama natafuta mke, lakini kwa sasa ni kwa ajili ya usafi na mapishi tu! Kama unamjua binti yeyote mwenye vigezo hivi na anatafuta kazi, niletee CV yake (au picha yake kwanza nione kama rangi imekubali).

Kazi ipo, mshahara ni makubaliano na mazingira ni rafiki sana!

Wako katika ujenzi wa Taifa.
 
Hupiki vichinchili Tena 😀 au umemaliza nakumbuka, na pia kule naona kimya 🥹
Mkuu nimefungiwa pm sijui shida nini aiseee
IMG_20260307_003000.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom