Habari zenu wanajamvi?
Natafuta generator ndogo ambayo itaweza kunisaidia kwa ajili ya kupata mwanga, kutumia ktk TV pamoja na kuwasha mashine ya kuvuta maji (katika kisima kirefu - borehole), n.k.
Niliambiwa kuwa nzuri ni zile za 5KV.
Pia ninahitaji generators zinazotumia mafuta kidogo sana na zisizotoa sauti kubwa (zenye sound proof system) - kama zipo.
Nitazipata wapi kwa Dar na zinauzwa bei gani?