Natafuta Gari Saloon ya injini ndogo bei isizidi 4mil

Jiandae kuwa mteja wa garage mala kwa mala kwa hiyo bei yako
Ongeza dau utapata gari zuli lisilo na usumbufu
 
we hutaki gari utakuwa unataka bajaj sasa umekosea kuandika?gari kwa 4m upate wapi hiyo si hela ya kununua bajaj
 
wasikuvunje moyo, magari ya 4m yapo mengi na yanarun vizuri tu, kuna watu wengi wana magari wanashindwa kuyaendesha kwa sababu mbalimbali
nasema hivyo nina uhakika, wiki iliyopita jamaa yangu kapata gari ya 3.8m jamaa alikuwa kaipaki, na hiyo gari jamaa akaiendesha kutoka dar mpaka Mbeya bila tatizo wala service ya kihivyo

Ngangania sana upate toyota, ina spare nyingi na ziko cheap
 
wasikuvunje moyo, magari ya 4m yapo mengi na yanarun vizuri tu, kuna watu wengi wana magari wanashindwa kuyaendesha kwa sababu mbalimbali
nasema hivyo nina uhakika, wiki iliyopita jamaa yangu kapata gari ya 3.8m jamaa alikuwa kaipaki, na hiyo gari jamaa akaiendesha kutoka dar mpaka Mbeya bila tatizo wala service ya kihivyo

Dar - Mbeya ni chini ya km 1000. Kipimio cha gari zuri si kwenda umbali huo tu bila service. Kuna hatari ya kumpotosha mwuliza swali.
 
Kama ukikosa unayoitaka, njoo kwangu, nina Toyota Mark II Grande six cylinder, ipo katika hali nzuri tu. Nataka 6m tu (unaweza kuzungumza pia)
 
Ndugu gari ndogo aina gani? Beetle? Hyundai? Toyota? Nissan? Mitsubishi...au? Engine ndogo ipi? 1.2, 1.3, 1.4, 1.5 au 1.6? hujafafanua transmission Manual au Auto? Ya Petrol au Dizel. Pia ya mwaka gani :teeth:
 
Wasiliana na 0763 213630 ana Mark II 4 cylinder, ipo ktk hali nzuri sana. Anaiuza kwa 4.5M
 
Nakushauri usiwe na haraka gari ya bei hiyo unaweza kupata tena kutoka nje.
Na kama hujali kagua mwenyewe aina ya gari unalotaka kupitia Japanese used cars. Used Japan car exporters. Used Japanese car dealers. [ tradecarview ] halafu click advance search unajisevia mwenyewe achana na madalali na matapeli waliojaa kila kona. Tafuta wakala mzuri asiye na tamaa,print picha na aina ya gari peleka Tra wakupe makisio ya kodi na kama hujali ulizia zaidi na kwa Interpole kuepuka usumbufu usio na lazima.

Unaweza kupata gari chini ya dola 1000 kuwa makini acha papara utakatishwa tamaa
 
Ndugu usiwe na wasiwasi,kama unaye rafiki zanzibar au kama u anaweza nenda kule utapata gari nzuri sana kwa milioni 3,then hiyo milion moja unaitumia kusafirishia na kulipia difference a kodi huku dar!kila la heri ndugu
 
Toyo muundo wa gari lakini tairi tatu injini kama zile wanazoweka katika baiskeli inakufaa??No +255754144
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom