CoderM
Senior Member
- Jun 15, 2015
- 112
- 314
Habari zenu wanajamvi?
Mimi ni Mpambanaji(Muhitimu wa chuo kikuu UDSM) nilimaliza pale 2015. Nina miaka 35, nna familia ya mke na watoto watano. Kwa sasa niko Kilimanjaro.
Katika harakati nyingi nilizofanya (kilimo, ufugaji na graphics na web design) nilibahatika kununua gari aina ya toyota hiace (3L), na niliendesha kama daladala kwa takribani miaka miwili. Ile gari ilikua inanipa pesa nzuri ila bahati mbaya nilinunua kwa mtu ikiwa imetumika na injini ilikua ndogo kulingana na matumizi, kwa hiyo baada ya kupata hela kidogo ikaanza kunisumbua na matumizi ya matengenezo yakawa makubwa kuliko mapato.
Mwanzoni nilikua napiga ruti za vijijini ambapo kulikua na uhakika wa kulaza 50,000 mpaka 100,000 kwa siku baada ya kutoa matumizi ya kila siku. Lakini kutokana na ubovu wa gari ambao nilishindwa kuutatua kwa wakati kwa sababu kwanza nilikua mgeni kwenye mambo ya magari ya abiria lakini pia nilikosa fundi mzuri wa kutatua changamoto za gari.
Baada ya gari kunisumbua kwa muda mrefu, na ikawa haiwezi kazi baadae nikaamua kuiuza kutokana na stress za kuendesha gari bovu la abiria(nadhani hapa madereva wataelewa namaanisha nini?)
Nikaamua kuachana na mambo ya magari na kufungua ofisi lakini ni mwaka sasa naona kazi ya barabarani ilikua inanilipa kuliko hii ambayo biashara ni ngumu sana.
Kwa sasa nataka nirudi barabarani lakini nikiwa na gari mpya. Nina uwezo kukopesheka benki kwa hati ya nyumba lakini siwezi kwa sababu mimi ni muislamu na riba haifai katika dini.
Hivyo basi natafuta mtu ambae anaweza kufanya uwekezaji wa kununua/(au kama tayari analo ambalo liko kwenye hali nzuri sana) gari kama hiace(5L au 2RZ), ya mkataba, yaani ninakua nnalipa kidogo kidogo mpaka hela ikikamilika tuliyoelewana halafu gari linakua langu kama wanavyofanya kwenye boda na bajaji.
Nina uwezo wa kulipa 50,000 kila siku, 1,500,000 kwa mwezi, na 18,000,000 kwa mwaka. Mkataba natamani uwe kati ya miaka miwili na isizidi mitatu kutokana na hali na upya wa gari. Service zote za gari hazitamuhusu muwekezaji kwa kipindi chote cha mkataba.
Kutokana na harakati zangu nyingine ambazo nnaendelea nazo kila siku za kilimo na ufugaji nna weza kumaliza mkataba kabla hata ya muda tutakaopangiana.
Kama unayo gari(hiace 2RZ au 5L) yenye hali nzuri sana, au una uwezo wa kuwekeza au kuna mtu unamjua anaweza kuwekeza kwenye hili naomba uniwezeshe, tupunguze vijana wasio na ajira mtaani.
KUHUSU USALAMA WA UWEKEZAJI WAKO.
1. Gari italipiwa bima kubwa kwa kipindi chote cha mkataba (Bima ya ajali, wizi, au moto)
2. Gari itawekwa GPS na muwekezaji na ataweza kupata realtime location muda wowote atakae hitaji.
3. Gari itajidhamini kwa kuwa muekezaji atakua ni mmiliki halali wa hiyo gari mpaka mkataba utakapoisha.
4. Kama kutahitajika nnaweza kuweka hati ya nyumba kama sehemu ya dhamana.
Asanteni sana nawasilisha.
0761629511