pambana kwanza na hayo maisha mengine kabla hujawaza kuwa na kitu cha mtu.Huu sio mkopo wa kufilisi mtu, huu ni mkopo kazi. Vikishindikana mwenye mali yake anaichukua na mimi naendelea kupambana na maisha mengine.
Lizo mkristu vs Ustaadhi CoderMNdugu yangu kitu unachoitaji ni kikubwa sana alafu tayar umemkaba muwekezaji asipate faida asa uliposema mkataba uwe wa miaka miwili.Ebu vuta picha haice mpya 5L ukiagiza japan adi inafika mkoni mwako inaweza kukulamba 32-35milion apo akuna bima,vibali vya kazi alafu wewe unataka kwa mwaka umlipe mwekezaj 18milion au 36milio kwa miaka miwili na gar iwe yako (huu ni utapeli wa kimahesabu na ukweli ata bajaj huwez pata)
Wewe hufai kupewa gari kwa haya majibu yako ya udini. Hamia AfghanistanMko
Mkopo wa benk za kiislamu haujatimiza masharti ya mkopo wa kiislamu. Kwa sababu mkopeshaji sio mwenye kumiliki mali anayoikopesha. Kwahiyo zile ni riba zilizojificha kwenye kichaka cha faida.
wao ni wakopeshaji wa magari aina zote, na mashne za viwandan na vifaa vya kilimo.Fafanua kidogo ni wakina nani hao? Ni wauza magari au ni taasisi ya mkopo.
Vipi kama ikawa ni used tayari kwenye good condition halafu ikawa mkataba wa miaka mitatu nayo itakua utapeli? Au umeamua kuchagua upande wa kusapoti pointi yako.Ndugu yangu kitu unachoitaji ni kikubwa sana alafu tayar umemkaba muwekezaji asipate faida asa uliposema mkataba uwe wa miaka miwili.Ebu vuta picha haice mpya 5L ukiagiza japan adi inafika mkoni mwako inaweza kukulamba 32-35milion apo akuna bima,vibali vya kazi alafu wewe unataka kwa mwaka umlipe mwekezaj 18milion au 36milio kwa miaka miwili na gar iwe yako (huu ni utapeli wa kimahesabu na ukweli ata bajaj huwez pata)
Mzee watu hela hawana na watoto wakose??ila unapambana kuzaa sana mkuu..wewe utakuwa salafy
hakuna kitu ninachokidharau sana kama huna pesa halafu unazaaa sana..Mzee watu hela hawana na watoto wakose??
Ni hatari kwa uchumi ila ndio.hivyo watu wanajilipua mkuuhakuna kitu ninachokidharau sana kama huna pesa halafu unazaaa sana..
I like your replies 👍Vipi kama ikawa ni used tayari kwenye good condition halafu ikawa mkataba wa miaka mitatu nayo itakua utapeli? Au umeamua kuchagua upande wa kusapoti pointi yako.
Kutokua na pesa ni kwa kipimo gani? Kwa mfano kati ya watoto watano nilionao wanne wameanza shule na hakuna hata mmoja anaesoma st. kayumba. Kwa ufupi hela ya kukidhi mahitaji ya familia inapatikana lakini kupiga hatua kadhaa mbele ndio tunazifosi.hakuna kitu ninachokidharau sana kama huna pesa halafu unazaaa sana..
Wakiwa wao ni wamiliki, hapo hakuna riba ila kama na wao wananunua ndio wakupe ulipe kidogo kidogo hapo ndio riba inapatikana. Asante ngoja niwafuatilie nitaleta mrejesho.wao ni wakopeshaji wa magari aina zote, na mashne za viwandan na vifaa vya kilimo.
Riba lazma iwepo, maana mtaelewana mda wa kulipana
Umeeleza vizuri sana kama Mdomo, umenyookaHabari zenu wanajamvi?
Mimi ni Mpambanaji(Muhitimu wa chuo kikuu UDSM) nilimaliza pale 2015. Nina miaka 35, nna familia ya mke na watoto watano. Kwa sasa niko Kilimanjaro.
Katika harakati nyingi nilizofanya (kilimo, ufugaji na graphics na web design) nilibahatika kununua gari aina ya toyota hiace (3L), na niliendesha kama daladala kwa takribani miaka miwili. Ile gari ilikua inanipa pesa nzuri ila bahati mbaya nilinunua kwa mtu ikiwa imetumika na injini ilikua ndogo kulingana na matumizi, kwa hiyo baada ya kupata hela kidogo ikaanza kunisumbua na matumizi ya matengenezo yakawa makubwa kuliko mapato.
Mwanzoni nilikua napiga ruti za vijijini ambapo kulikua na uhakika wa kulaza 50,000 mpaka 100,000 kwa siku baada ya kutoa matumizi ya kila siku. Lakini kutokana na ubovu wa gari ambao nilishindwa kuutatua kwa wakati kwa sababu kwanza nilikua mgeni kwenye mambo ya magari ya abiria lakini pia nilikosa fundi mzuri wa kutatua changamoto za gari.
Baada ya gari kunisumbua kwa muda mrefu, na ikawa haiwezi kazi baadae nikaamua kuiuza kutokana na stress za kuendesha gari bovu la abiria(nadhani hapa madereva wataelewa namaanisha nini?)
Nikaamua kuachana na mambo ya magari na kufungua ofisi lakini ni mwaka sasa naona kazi ya barabarani ilikua inanilipa kuliko hii ambayo biashara ni ngumu sana.
Kwa sasa nataka nirudi barabarani lakini nikiwa na gari mpya. Nina uwezo kukopesheka benki kwa hati ya nyumba lakini siwezi kwa sababu mimi ni muislamu na riba haifai katika dini.
Hivyo basi natafuta mtu ambae anaweza kufanya uwekezaji wa kununua/(au kama tayari analo ambalo liko kwenye hali nzuri sana) gari kama hiace(5L au 2RZ), ya mkataba, yaani ninakua nnalipa kidogo kidogo mpaka hela ikikamilika tuliyoelewana halafu gari linakua langu kama wanavyofanya kwenye boda na bajaji.
Nina uwezo wa kulipa 50,000 kila siku, 1,500,000 kwa mwezi, na 18,000,000 kwa mwaka. Mkataba natamani uwe kati ya miaka miwili na isizidi mitatu kutokana na hali na upya wa gari. Service zote za gari hazitamuhusu muwekezaji kwa kipindi chote cha mkataba.
Kutokana na harakati zangu nyingine ambazo nnaendelea nazo kila siku za kilimo na ufugaji nna weza kumaliza mkataba kabla hata ya muda tutakaopangiana.
Kama unayo gari(hiace 2RZ au 5L) yenye hali nzuri sana, au una uwezo wa kuwekeza au kuna mtu unamjua anaweza kuwekeza kwenye hili naomba uniwezeshe, tupunguze vijana wasio na ajira mtaani.
KUHUSU USALAMA WA UWEKEZAJI WAKO.
1. Gari italipiwa bima kubwa kwa kipindi chote cha mkataba (Bima ya ajali, wizi, au moto)
2. Gari itawekwa GPS na muwekezaji na ataweza kupata realtime location muda wowote atakae hitaji.
3. Gari itajidhamini kwa kuwa muekezaji atakua ni mmiliki halali wa hiyo gari mpaka mkataba utakapoisha.
4. Kama kutahitajika nnaweza kuweka hati ya nyumba kama sehemu ya dhamana.
Asanteni sana nawasilisha.
0761629511
View attachment 3561584
Mkuu huyo jamaa achana naye, endelea na maisha yako ya kupambanaKutokua na pesa ni kwa kipimo gani? Kwa mfano kati ya watoto watano nilionao wanne wameanza shule na hakuna hata mmoja anaesoma st. kayumba. Kwa ufupi hela ya kukidhi mahitaji ya familia inapatikana lakini kupiga hatua kadhaa mbele ndio tunazifosi.