Kiongozi hata uwe na magari kumi,
Hata uwe na uzoefu wa miaka kumi.
Gari jipya ni jipya tu hata likiwa mkweche.
Matatizo mengi ya barabarani kwenye nchi yetu hii ya Tanzania yanasababishwa na haraka.
Kama unahofia kupigwa pasi pangilia route zako vizuri utoke mida ambayo hamna foleni mpaka utakapolizoea gari lako.
Kuna mdau kashauri ujichange mpaka 2.5, hapo mimi ningeshauri katika hiyo 1.5 utoe kama laki nne. Uende kujifunza udereva kwenye chuo sahihi, lazima kulikua na bajeti ya mafuta.
Tumia bajeti hiyo ndani ya mwaka utakua unakaribia 2 fulani hivi.
kumbuka usalama ni muhimu kwako na kwa wenzio. Usijifunzie gari barabarani bila taratibu sahihi.
Kwa kumalizia kuna sehemu nilisoma, takwimu zinaonesha wamiliki wengi wa magari kwa mara ya kwanza, mara yao yanahusika kwenye ajali (kubwa au ndogo) ndani ya miezi mitatu ya kwanza.
Nyingi sio wao waliosababisha, kwa hiyo hata ukiwa makini na mwenye uzoefu haimaabishi utakaye mruhusu atoke na gari lako atalirudisha salama