Natafuta gari aina ya funcargo!!

kubwa_Lao

JF-Expert Member
Dec 12, 2015
934
1,183
1596449808597.png

Habari za asubuhi wadau,

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza, nahitaji funcargo ingawa bajeti yangu ya 5M ni ndogo lkn ndio nahitaji gari hiyo iwe kuanzia namba C iliyo karibu na D na kuendelea.

Wadau mie hiyo ndio itakua gari yangu ya kwanza, sijawahi kumiliki gari hivyo mwenye nalo tafadhali tuwasiliane, pamoja kuwa ndilo gari ninalohitaji pia nakaribisha maoni au msaada zaidi wa mawazo ya gari ipi ni nzuri kutokana na bajeti yangu hiyo.

Passo nilikua naipenda lkn kutokana na maoni ya kitaalamu niliyoyasoma humu naona passo haitanifaa kwa kazi zangu za humu mjini lkn pia na kwenda mikoani.

Pia nitashukuru sana kama nitapata uzuri na ubaya wa funcargo.

Natanguliza shukrani.
 
funcargo ina shepu mbaya, alafu haipo imara! kiukwel sikushauri ununue funcargo
- kama unataka ya cc ndogo chukua vitz utafurah na roho yako, ni ngumu na zinavumilia shida zote
- kama unataka gari yenye cc ndogo na ipo juu basi chukua Ractis
Yah huenda ikawa kweli ina shepu mbaya, si unajua tena mkuu uzuri wa kitu uko machoni kwa mtazamaji......
Vitz mie hainivutii kabisa ndio maana hata sijaitaja kabisa.
Racti..... Naipenda ila tatizo bei mkuu.
Asante sana kwa ushauri mkuu
 
Funny Car go now.... Aisee.. Achana na hicho kidude. Kwa nini usiongezee ongezee ukanunua hata Rav 4? Mi gar chini ya CC 1500 Huwa naona ni sawa na Bajaji tu.

We una uzito gani?hutegemei kunenepa?mkeo?watoto? Kigari hicho hakina nguvu kuna jamaa aliomba nimsaidie kukitoa bandarin nimpelekee kwake nilimgomea nikampa fundi wangu hiyo kazi.

Nliona aibu sana nionekane kwenye funcargo. Jamaa naye akakiendesha week mbili akakiuza anasema ni cha aibu. Akanunua noah.
 
Funny Car go now.... Aisee.. Achana na hicho kidude. Kwa nini usiongezee ongezee ukanunua hata Rav 4? Mi gar chini ya CC 1500 Huwa naona ni sawa na Bajaji tu. We una uzito gani?hutegemei kunenepa?mkeo?watoto? Kigari hicho hakina nguvu kuna jamaa aliomba nimsaidie kukitoa bandarin nimpelekee kwake nilimgomea nikampa fundi wangu hiyo kazi. Nliona aibu sana nionekane kwenye funcargo. Jamaa naye akakiendesha week mbili akakiuza anasema ni cha aibu. Akanunua noah.
Shemeji hajakufukuza kwake tu?
 
Mimi nataka kujua tatizo la rav4 ya1998 katika reverse gear inakuwa free hairudi nyuma, ni automatic gear . Tatizo ni lipi?
 
Kwa kweli watu tunatofautina sana, kwangu mm FunCargo ni moja ya gari nzuri sana nitawashangaza kwa wale wanene fun cargo unakaa vizuri comfortable kuliko hata carina TI, nafasi kubwa nyuma kwa mizigo kwa wale wajasiriamali na wakulima na wafugaji - mayai, mbogamboga, maziwa ya kutembeza, marobota mitumba kwa funCargo umefika.

Engine ndogo na zipo aina mbili ya cc1290 na cc1490 mafuta kiduchu iko juu kuliko punda nyingine inayoitwa PROBOX
 
Salaam,

Toyota Funcargo ni moja kati ya magari yenye sifa kubwa kabisa kutoka kwenye kampuni ya toyota. Sifa hio nayo ni utumiaji mdodo wa mafuta.

Hizi gari kwakweli zinasifika sana juu ya upande huo wa matumizi madogo ya mafuta, infact kuliko kununua vitz, ni bora hizi. Maana ina nafasi ya kutosha kabisa ndani, na kikubwa zaidi zile siti (za nyuma ) unaweza kuzilaza na ukapata nafasi kubwa zaidi kuweza kuwekea vitu.

MATATIZO YAKE ;

Hakuna gari ambayo hinga matatizo, kila gari inaudhaifu wake.

Hizi gari, udhaifu wake ni;

> Shock absobers
> Bushes
> Bearing

Lakini pamoja na hayo yote, upatikanaji wa spare parts zake ni mkubwa sana, spare parts zake ziko kwa wingi mno.

Ikiwa utahitaji, karibu tuwasiliane. Kwa Tshs 8,500,000 ninaweza kukuletea kutoka japan, mpaka kukabidhi mkononi , utakacholipia ni bima tu basi.


Ahsante
 
Na mimi nataka kupata ufafanuzi wa gari ndogo iitwayo Duet ubora na udhaifu wake. Nataka kuinunua kwa sifa ya matumizi madogo ya mafuta, je ni kweli?
 
Back
Top Bottom