Natafuta dawa ya kienyeji ya kutibu malaria

Abbasfarudume

JF-Expert Member
Feb 14, 2017
1,625
1,325
Wakuu bila kuchelewa na kumung'unya mate na maneno midomoni, nilikuwa naomba ushauri na maelekezo kutoka kwenu, bila mzaha wala jokes, kikubwa zaidi nilikuwa naomba mnishauri dawa ya kutibu malaria za kienyeji.

Ipi dawa ilio bora, maana hizi dawa za hospital, nahisi kama hazisaidii na zingine ukizitumia baada ya upate nafuu ya kupona ndio zinakuchosha kabisa mwili saa nyingine mpaka appetite ya kula inapotea mdomoni.

Sasa kama yupo mtaalam wa dawa ya malaria za kienyeji naomba anielekeze nawasilisha huu uzi kwenu wakuu kwa heshima na taadhima itifaki imezingatiwa wakuu.
 
sasa picha zako zinahusiana nini na dawa?

Anyway katafute mlonge longe unapatikana mikoa ya pwani mpaka morogoro!
chuma majani yake kausha halafu saga!
kunywa glas moja mara3,maji ya vugu vugu!
Ni kinga tosha
 
Aloe vera .Usiweke maji. Badala yake weka asali mbichi. Kunywa vijiko vitatu kutwa mara tatu.
 
piga aloe vera kuna jamaa anauza ukipiga chupa mbili UTI,na TYPHOID pia utazisikia kwa jirani tuu,ila ukoma na dozi
 
Wakuu bila kuchelewa na kumung'unya mate na maneno midomoni, nilikuwa naomba ushauri na maelekezo kutoka kwenu, bila mzaha wala jokes, kikubwa zaidi nilikuwa naomba mnishauri dawa ya kutibu malaria za kienyeji.

Ipi dawa ilio bora, maana hizi dawa za hospital, nahisi kama hazisaidii na zingine ukizitumia baada ya upate nafuu ya kupona ndio zinakuchosha kabisa mwili saa nyingine mpaka appetite ya kula inapotea mdomoni.

Sasa kama yupo mtaalam wa dawa ya malaria za kienyeji naomba anielekeze nawasilisha huu uzi kwenu wakuu kwa heshima na taadhima itifaki imezingatiwa wakuu.
0787986992 Mtafute huyu jamaa kama upo Dar
 
piga kitu salehe la Ishofu ama Aloe Vera ukichanganya na Asali Hatari sana
 
Kuna shamba la NIMR lipo Tanga kula wameotesha mimea ya dawa mbalimbali.

Nko mbali kwa sasa labda uni pm baada ya mwezi nitakutumia picha na majina ya izo dawa.
 
sasa picha zako zinahusiana nini na dawa?

Anyway katafute mlonge longe unapatikana mikoa ya pwani mpaka morogoro!
chuma majani yake kausha halafu saga!
kunywa glas moja mara3,maji ya vugu vugu!
Ni kinga tosha
Ahsante mkuu kwa ushauri, hila pic zisikustue sana sometime ni pozz tu
 
Back
Top Bottom